26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

MADIWANI DODOMA WAMNG’OA MEYA WAO

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

HATIMAYE  Baraza  la Madiwani la Manispaa ya Dodoma limemng’oa  Meya wa Manispaa hiyo, Japhari Mwanyemba (CCM), kwa tuhuma za kutafuna Sh milioni 30 za mradi wa maji katika eneo la Zuzu  katika manispaa hiyo.

Fedha hizo zilizotolewa na Ubalozi wa Japani kwa aliyekuwa Mke wa Waziri Mkuu, Tunu Pinda kwa ajili ya mradi huo.

Madiwani hao ambao kwa pamoja walipiga kura za kutokuwa na imani na Mwanyemba katika kikoa maalumu cha baraza hilo kilichofanyika jana  mjini hapa.

Zoezi hilo ambalo liliongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma,  Godwin Kunambi,  akishirikiana na Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Jumanne Ngede.

Pia zoezi hilo lilishuhudiwa na Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde, Mbunge wa Viti Maalumu Felister Bura na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme.

Sekeseke hilo lilianza baada ya mkurugenzi kumaliza kusoma ripoti ya tume iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana kuchunguza  fedha za mradi huo wa maji kutowaridhisha baadhi ya madiwani.

Mkurugenzi huyo alitumia zaidi ya saa nane kuisoma ripoti hiyo huku wajumbe wakiwa wapole na wengine wakionekana kuguswa kwa hisia kali.

Naibu Meya Ngede aliagiza kupigwa kwa kura za siri ambapo kati ya madiwani 56 waliohudhuria baraza hilo 43 walipiga kura ya kutokuwa na  imani na mwenyekiti huyo.

Akitangaza matokeo Mkurugenzi wa manispaa hiyo Kunambi alisema madiwani 8 waligomea zoezi hilo na kutoka nje huku wane wakipiga kura ya kuwa na imani na meya huyo na 43 wakiunga mkono kumng’oa.

“Natangaza kwa mujibu wa kanuni za Halmashauri kifungu namba 4 kanuni ndogo ya nane kuanzia mida hii majira ya saa 8.30 mchana  waheshimiwa madiwani natangaza rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma sio Mstahiki tena,’’alisema Kunambi huku akishangiliwa.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,371FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles