23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

MADIWANI CHADEMA WATILIWA SHAKA URAIA WAO   

 

Na Gurian Adolf-Sumbawanga

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Rukwa, kimeiomba Idara ya Uhamiaji mkoani humo kufanya kazi zake kwa weledi bila kuburuzwa na wanasiasa tofauti ili kuepuka mvutano usiokuwa na sababu.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Rukwa, Sadrick Malila, alisema chama hicho kinaiomba idara hiyo kubadilika kutokana na kitendo cha kuwakamata madiwani wa Kata ya Korongwe, Venance Bamilitwaye na Ruben Mkisi wa Kata ya Mkinga Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, wakiwatuhumu kuwa si raia wa Tanzania.

Akizungumza na gazeti hili, Diwani Bamilitwaye, alisema mwaka 2005, aligombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu kupitia Chadema hakushinda na hakukuwa na shida yoyote na uraia wake haukutiliwa mashaka.

Alisema mwaka 2010, aliingia tena katika kinyang’anyiro na akafuata taratibu zote na hakuwekewa pingamizi na alishinda katika kata hiyo ndipo tabu ilipoanza kwani alikamatwa nakufikishwa mahakamani kuwa si raia wa Tanzania.

Naye Diwani Mkisi, alisema baada ya kushinda uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, iliibuka hoja kuwa si raia wa Tanzania ambapo alikamatwa na kufikishwa mahakamani, lakini alishinda kesi.

Alisema anashangazwa na Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa, Carlos Haule, kuwapelekea wito wa kufika ofisini kwake.

Naye Katibu wa Madiwani wa Chadema wa kanda hiyo, Joseph Nzala, alisema vitendo vinavyofanywa na idara hiyo ni vya unyanyasaji.

Kwa upande wake, Haule alipozungumza na gazeti hili alikiri kuwaita madiwani hao na kuwataka wafike ofisini kwake leo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,244FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles