25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Madiwani Buchosa waridhia kuhamia Mkoa wa Geita

Anna Ruhasha, Sengerema

Madiwani wa Halmashauri ya Buchosa wameridhia kuhamia mkoani Geita kwa sharti la Halmashauri hiyo kupandishwa kuwa Wilaya na kuongezwa Tarafa, Vijiji na Kata.

Hatua hiyo imekuja katika mkutano maalum wa madiwani wa Halmashauri hiyo katika kujadili agenda ya maombi ya kuanzishwa mkoa mpya wa Chato kwa kumegwa Jimbo la Buchosa.

Awali mkurungenzi wa Halmashauri hiyo, Paulo Malala ametaja faida za kurudi mkoani Geita ikiwa ni pamoja kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi kutokana na kupungua kwa umbali ambapo kutoka Buchosa hadi Mwanza ni Km 110 huku umbali wa Buchosa kwenda Geita ni Km 58 nakwamba hali hiyo itasaidia huduma kupatikana kwa urahisi na kuwafikia wananchi kwa muda mfupi.

Malala ameongeza kuwa mbali na umbali pia maoni ya kamati ya Fedha ,Utawala na Mipango baada ya kujadili faida na athari za Halmashauri ya wilaya ya Buchosa kuhamia mkoani Geita ili kuwezesha mkoa wa Chato kuanziashwa , iliridhia kumegwa kwa Jimbo la Buchosa na kuwa sehemu ya mkoa wa Geita endapo Halmashauri hiyo itapewa hadhi ya kuwa Wilaya yenyewe na mamlaka kamili.

Pia amesema Halmashauri hiyo ikipata fursa itaongeza huduma za kijamii Kkma vile Mahakama, Kituo Kikuu Cha Polisi, Magereza, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kurahisisha pia upatikanaji wa huduma nyingine za kijamii ambazo hazikiwepo eneo hilo.

Aidha, baadhi ya madiwani wakizungumza uamuzi huo akiwemo, Zena Jacobo na Dotto Bulunda diwani kata Kafunzo kwaniaba ya wenzao wemeunga mkono jambo hilo na kusema kuwa wapo tayari kuhamia mkoani Geita.

Hata hivyo katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Sengerema, Barnabas Nyerembe pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Idama Kibanzi mwisho wa kikao hicho walipongeza kwa maoni yao ya kutaka kuhamia mkoani Geita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles