23.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 10, 2022

Madereva watakiwa kujiepusha na pombe, dawa za kulevya

Sheila Katikula-Mwanza

SERIKALI imewataka madereva kuacha kutumia dawa za kulevya, lugha chafu, pombe wakati wa kazi na badala yake kufanya kazi kwa weledi, kujitambua, uadilifu na utii kwa kufuata sheria za barabarani bila shuruti.

Rai hiyo ilitolewa jana na mgeni rasmi kutoka Kituo cha Polisi cha Kata ya Pamba, Peter Maiga wakati wa kikao cha madereva na makondakta Mkoa wa Mwanza cha kutambulisha viongozi wapya pamoja na kupanga mikakati ya kuimarisha chama chao.

Maiga alisema ni kosa kwa dereva yeyote kujihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya, pombe na kutoa lugha chafu kwa abiria na kufanya hivyo Jeshi la Polisi halitafumbia macho. Alisema kila dereva ana wajibu wa kutoa taarifa kituo cha polisi pindi anapofanyiwa fujo na abiria, huku wakitakiwa kuvaa sare za kazi safi na kuacha kujichukulia sheria mkononi pindi wanapotofautiana na wateja wao

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,395FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles