30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Madereva wa malori wailalamikia manispaa 

Na AVELINE KITOMARY DAR ES SALAA


MADEREVA wa malori ya kusafirisha mafuta wanaoegesha magari yao   Keko Mwanga B  Dar es salaam, wameilalamikia  Manispaa ya Temeke kuwatoza ushuru mkubwa wakati mazingira hayo hayana usalama na huduma sahihi kwa ajili ya maegesho.

Wakizungumza na MTANZANIA, madereva hao waliiomba  manispaa hiyo kutenga eneo maalum kwa ajili ya maegesho ya magari na kuwawekea mazingira salama na utaratibu sahihi wa ulinzi ili walipe ushuru halali.

“Manispaa inatutoza Sh 2,000 kwa ajili ya maegesho ya magari huku hawajaweka mazingira sahihi ya kuegesha magari.

“Hapa ni barabarani si maegesho hivyo sisi madereva ndiyo tunaoumia.

“Fedha  za ushuru hazitoki kwa mabosi wetu tunalipa wenyewe na ukikataa kulipa gari linafungwa minyororo.

“Tunataka manispaa itutengee maeneo maalum kwa ajili ya maegesho ya magari, hapa usalama ni mdogo pia hakuna huduma muhimu na utaratibu unaoeleweka,” alisema Sadick Masoud.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles