31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Madereva sugu 537 wafungiwa leseni

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

JUMLA ya madereva 537 wamefungiwa leseni zao za udereva katika kipindi cha Januari hadi Septemba 2021 baada ya kuonekana  kuwa sugu  kwa kufanya makosa  hatarishi  barabarani.

Madereva 472 wamefikishwa mahakamani, huku 107,146 wamelipishwa faini za hapo kwa hapo, wakati 1,720 wakipewa onyo.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, SACP Wilbroad Mutafungwa mbele ya Rais Samia Suluhu Hassani wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama leo Novemba 23,2021 mkoani Arusha.

SACP Mutafungwa amesema  hatua hizo ni katika usimamizi wa  kisheria  na kanuni  kwa madereva kwa kuzingatia makosa hatarishi  yanayosababisha madhara makubwa kama kuendesha huku dereva anaongea na simu, ulevi na mwendokasi, kutofunga mkanda na ukosefu wa viti vya kuwalinda watoto ndani ya gari.

Hata hivyo amesema  hali ya usalama barabarani inazidi kuimarika kutokana na ajali za barabarani kuendelea kupungua.

Akitoa takwimu za matukio ya ajali za barabarani  za kipindi cha miaka minne iliyopita,  amesema hali hiyo pia imechangiwa na uotoaji wa elimu  kwa njia mbalimbali ikiwamo vipindi vya redio na runinga.

Ametoa takwimu za ajali  zinazoanzia Januari hadi Septemba kwa kila mwaka kuwa “Mwaka 2018  jumla ajali zilikuwa  3,732,  mwaka 2019  ajali ni  2,704,  hivyo tumefanikiwa kupunguza matukio ya  ajali 1,028 sawa na asilimia 27.5.

Rais Samia Suluhu Hassan, akihutubia katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyoanza leo Novemba 23, 2021  kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha

“Vifo vilivyotokana na ajali katika kipindi hicho, ni mwaka 2018 vifo ni 1,788 na mwaka 2019 ni 1,440, hivyo tumepunguza  vifo 348 sawa na asilimia 19.5.

“Majeruhi mwaka 2018 walikuwa 3,746, mwaka 2019 majeruhi  2,830, hivyo tumefanikiwa kupunguza majerhi 912 sawa na asilimia 24.3.

“Mwaka 2019/2020 ulinganisho, matukio ya ajali yalikuwa 2,704, mwaka 2020, 1,714, hivyo tukawa tumefanikiwa kupunguza matukio 990 sawa na asilimia 36.6. Mwaka 2019 vifo vilikuwa 1,440  mwaka 2020 , vifo 1,270,  kukawa na punguzo la  vifo 170, sawa na asilimia 11.8.

“Majeruhi mwaka 2019  walikuwa 2,830, mwaka 2020 walikuwa  2,126, tumefanikiwa kupunguza 708 sawa na asilimia 25.0.

Katika kipindi cha Januari hadi Septemba 2020 ajali ni 1,388,  mwaka 2021 ajali   1,187, hivyo tumefanikiwa kupunguza ajali  201 sawa na asilimia 14.5.

“Januari hadi Septemba mwaka 2020, vifo vilikuwa  949, 2021 ni vifo 900,  tumepunguza vifo 49 sawa na asilimia 5.2.

“Majeruhi mwaka 2020 walikuwa  1, 672, mwaka 2021  katika kipindi hicho, majeruhi 1,405, hivyo tumefanikiwa kupunguza  267 sawa na asilimia 16.0, “

Aidha ametaja baadhi ya sababu za ajali za barabarani kuwa ni pamoja na makosa ya kibinadamu kama vile ni ulevi, mwendokasi, uzembe wa madereva na watembea kwa miguu, pia madereva wa pikipiki kutokuvaa kofia ngumu.

Ameeleza  kuwa  nyingine ni ubovu wa vyombo vya moto, utelezi, mvua kubwa, ukungu na miundombinu ya barabara.

Pia amemuomba Rais Samia kupatiwa vifaa vya kisasa vya kusaidia kukabiliana na ajali za barabarani ikiwamo vifaa vya kisasa vya ukaguzi wa magari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles