28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Madeni ya muda mrefu kwa makandarasi kulipwa mwezi huu

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Serikali imesema kila mwezi inatenga sh bilioni 70 kulipa madeni ya makandarasi huku Sh bilioni 50 zikielekezwa kwa makandarasi wazawa na kuwahakikishia kuwa hadi mwishoni mwa 2023 itamaliza madeni yote ya muda mrefu.

Ahadi hiyo ilitolewa Desemba 8,2023 na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Ludovick Nduhiye kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi, wakati wa uzinduzi wa Chama cha Umoja wa Makandarasi na Watoa Huduma Tanzania (Tucasa).

Amesema wanadaiwa karibu Sh bilioni 600 lakini kipaumbele kimelekezwa kwa makandarasi wazawa na kuwataka kufanya kazi kwa umahiri na uaminifu ili kuleta tija katika miradi wanayokabidhiwa.


“Hakikisheni mnaweka mipango thabiti ya kusimamia makandarasi ili mfanye kazi kwa uzalendo na weledi. Chunguzaneni ili kuhakikisha mnadhibiti wanaochafua jina la makandarasi wazawa kwa kazi zao kuwa duni.

“Mkipewa miradi mtembee pamoja na epukeni vishawishi wakati wa kupata mradi hasa rushwa,” amesema Nduhiye.

Aidha amesema sh bilioni 600 zilizotengwa kwa ajili ya kukarabati na kutengeneza barabara zitaelekezwa kwa makandarasi wazawa.

Amesema katika miradi minne ya barabara ambayo kila mmoja una urefu wa kilomita 50 utaelekezwa kwa makandarasi wazawa huku makandarasi wanawake wakipewa kilomita 20 kila mradi.

Mwenyekiti wa Tucasa, Samuel Marwa, amesema malipo ya makandarasi yamekuwa yakichukua muda mrefu hadi miaka miwili na kuiomba Serikali waruhusiwe kulipa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) baada ya kuikusanya kutoka kwa mlipaji.

“Malipo ni kipengele cha lazima katika kukua kwa mkandarasi, hatuwezi kusema tunakuza wazawa ikiwa hatutaweka mikakati ya kuwalipa kwa wakati.
Tunapendekeza kuanzishwa kwa ‘payment guarantee’ ili uhakika wa malipo uwepo na miradi ikamilike kwa muda na kwa gharama nafuu.

“VAT ni eneo la kuliangalia upya hususan kwenye biashara ya ukandarasi maana ni tofauti na biashara ya kuuza bidhaa. Ukimkata mkandarasi VAT kabla hajalipwa unazidi kumpunguzia nguvu ya kuendelea kufanya kazi,” amesema Marwa.

Amesema pia vigezo vya zabuni vinavyotolewa ili kupata kazi ni kikwazo kikubwa katika ukuaji wa mkandarasi wa ndani.

Mwenyekiti huyo ameshauri watoa kazi wasilazimishe dhamana za benki badala yake waache mkandarasi achague kama ni benki au bima na kuingizwa kwenye mikataba ya umma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles