32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 1, 2023

Contact us: [email protected]

Madee ashindwa kutimiza ahadi yake

Madee-ndingaNA HERIETH FAUSTINE

MSANII wa Bongo Fleva nchini, Hamadi Ally ‘Madee’, ameshindwa kutimiza ahadi yake ya kuchoma gari lake kama alivyoahidi kwamba angelichoma kwa moto kama timu anayoshabikia ya Arsenal ya Uingereza ingeshinda usiku wa juzi.

Katika mchezo huo Arsenal ilifungwa 1-0 na Chelsea huku bao hilo la ushindi likifungwa na Diego Costa na ahadi kushindwa kutekelezwa na msanii huyo aliyejinadi kabla ya mechi hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Hata hivyo, baada ya kushindwa kutekeleza ahadi hiyo aliwaambia mashabiki wake kupitia ukurasa wake wa twitter kwamba hajafikia utajiri wa kuchoma gari lake na hata kama angekuwa tajiri wa aina gani asingechoma gari hilo kama alivyoahidi.

“Sina utajiri huo mpaka kufikia hatua ya kuchoma gari na hata kama ningekuwa tajiri vipi nisingefanya upumbavu huo,” aliandika Madee na kuzua mapokeo tofauti kwa mashabiki wake huku wengine wakiwaonya kutoa ahadi mbalimbali wasizoweza kuzitimiza.

Baadhi ya mashabiki na wadau wa sanaa nchini walionya wasanii kujihusisha na ahadi wakati hawana uwezo wa kuzitekeleza kwa kuwa watakuwa hawana tofauti na wanasiasa wanaoahidi bila kutimiza ahadi zao.

“Kipindi cha uchaguzi kuna wasanii mbalimbali waliingia katika ahadi tena kubwa na za ajabu nyingine kuzieleza hapa, ni aibu wakiahidi bila kujali kuna kushindwa na kushinda wakaamini kushinda kwa asilimia 100 na leo wakikumbushwa ahadi zao wanatukana na kuanzisha ugomvi,’’ alieleza mdau huyo aliyejitambulisha kwa jina la Ali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles