31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MADARAKA NYERERE ATAKA VIFAA VYA NISHATI KUFUTIWA KODI

Na RAPHAEL OKELLO


KAIMU Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali  la Global Resource Alliance, Madaraka Nyerere, ameiomba serikali kupunguza kodi  katika bidhaa zinazotengeneza  nishati  ya jua.

Alisema hatua hiyo itawawezesha wananchi    vijijini kupata nishati hiyo na hivyo kupungu za matumizi ya kuni na mkaa inayochangia kuharibu misitu.

Alikuw akizungumza hivi karibuni   katika wiki ya maadhimisho  ya mazingira iliyofanyika kitaifa  wilayani hapa.

Madaraka  alisema shirika lake kwa kushirikiana na Kampuni ya GoSol Ltd kutoka    Finland  limebuni jiko la kutumia mionzi ya jua.

Alisema  jiko  hilo   litakuwa   ukombozi kwa wajasiriamali wadogo vijijini ambao  hawana uwezo  wa kumudu gharama za umeme, mafuta na gesi.

Akifafanua  faida ya jiko  hilo  linalotumia  vioo  vya  kawaida kukusanya  mionzi  ya jua, Meneja  Mradi  wa GoSol  kutoka Finland, Heikki  Lindfors, alisema  jiko hilo  ni ukombozi  kwa wakazi wa vijijini  zaidi ya bilioni tatu duniani.

Alisema jiko hilo  linaweza  kuokoa zaidi ya tani tisa ya miti  inayokatwa kwa mwaka duniani.

“Teknolojia  hii  tumekwisha kuieneza  katika  nchi mbalimbali duniani kama vile Nigeria, India na Kenya.

“Tanzania tumeanzia  hapa  Musoma mkoani Mara…  teknolojia  hii  itawasaidia vikundi vya  kina mama  ambao wana kazi kubwa  za uhitaji  wa nishati ya jua,” alisema Lindfors.

Alisema  jiko  hilo  lina  uwezo wa  kupika  vyakula  mbalimbali     na kukausha   karanga, kubani   kanyama,  kukausha ndizi  na kupata unga, kukausha    mihogo  na mitama na   lina   uwezo wa  kuoka   unga  wa mikate  wenye uzito  wa kilo 10.

Monica Macha, mjasiriamali  kutoka kikundi cha Alpha Alliance cha Musoma kilichoanza kutumia  teknolojia hiyo, alisema   kabla  ya kutumia jiko hilo walikuwa  wanatumia debe moja la mkaa kwa siku katika kuoka mkate au chapati jambo  ambalo kwa sasa ni ndoto kwao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles