24.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Madaktari wazungumzia wenzao waliougua corona nchini

Aveline Kitomary -Dar es salaam

CHAMA cha Madaktari Tanzania (MAT) kimesema madaktari walioambukizwa virusi vya corona wamepona na kwamba maambukizi ya ugonjwa huo nchini yemepungua hadi kufikia asilimia 10 kulingana na sampuli za damu zilizopimwa kuanzia mwanzani mwa mwezi huu.

Licha ya kutoa kauli hiyo, chama hicho kilisema hakiwezi kutoa takwimu za wahudumu wa afya waliopata ugonjwa huo kwa sababu za kimaadili.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Rais wa MAT, Dk. Elisha Osati, alisema idadi ya wagonjwa imepungua kwa kiasi kikubwa katika vituo vya kutolea huduma ambapo awali katika miezi ya Machi na Aprili waliofika na kupimwa sampuli walikuwa asilimia 90.

“MAT kwa kushirikiana na wataalamu katika vituo vya kutolea huduma nchini tumefanya tathmini juu ya mwenendo wa ugonjwa wa Covid-19 na kugundua idadi ya wagonjwa imepungua kwa kiasi kikubwa katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma.

“Idadi ya wagonjwa imepungua kwa kiasi kikubwa ndani ya jamii kwa kuangalia idadi ya simu zilizopigwa kwa kuuliza na kuomba msaada wa kitaalamu juu ya wagonjwa wenye dalili za Covid-19 na wanaougua. Idadi ya vifo vinavyodhaniwa kusababishwa na ugonjwa huo imepungua pia.

“Ugonjwa huo ulipoingia wapo baadhi ya wahudumu wa afya ambao wameugua na wamepona na kurejea makazini ili kuendelea kutoa huduma kama kawaida,” alieleza Dk. Osati.

Aidha aliwataka wagonjwa waliopo majumbani kwa matatizo ya ugonjwa huo au wagonjwa mengine waende hospitali wakahudumiwe kwani ugonjwa wa Covid-19 umepungua kwa kiasi kikubwa.

“Wagonjwa wengi wanaougua magonjwa mengine niwatoe hofu kuwa ugonjwa wa Covid-19 umepungua, mfike katika vituo vya afya mhudumiwe,” alisema Dk. Osati.

Pia alisema upatikanaji wa vifaa tiba ulikuwa ni changamoto ya dunia nzima kwa ugonjwa huo uliokuja kwa ghafla, hivyo Serikali na wadau mbalimbali walijitokeza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuhakikisha wahudumu wa afya wanakuwa salama.

Aidha Dk. Osati alimpongeza Rais Dk. John Magufuli kwa kuwaongoza Watanzania vizuri katika kipindi kigumu na kutoa mwelekeo unaofaa zaidi.

Kwa upande wake, Rais mteule wa MAT, Dk. Shadrack Mwaibambe, alisema katika kipindi hiki cha kukabiliana na corona, baadhi ya watu wamepona kwa tiba mbadala ikiwemo tangawizi, malimao, vitunguu swaumu na ndimu kutokana na vitu hivyo kusaidia katika mfumo wa hewa na damu.

“Ugonjwa huu unapoingia damu huganda, hivyo kupitia tangawizi inasaidia kuyeyusha damu ili iweze kukabiliana na vijidudu,” alisema Dk. Mwaibambe.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

12,054FansLike
2,941FollowersFollow
18,400SubscribersSubscribe
- Advertisement -spot_img

Latest Articles