32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Madaktari watoa tahadhari za kiafya ongezeko la joto

AVELINE KITOMARY – DAR ES SALAAM

SIKU chache baada ya Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kutangaza hali ya joto kali  nchini, madaktari bingwa wametoa ushauri kwa wananchi kuacha matumizi ya vilevi na mazoezi mazito yanayoweza kusabisha mwili kuchemka na kuongeza kiwango cha joto na hivyo kupata madhara katika viungo hasa moyo.

Madaktari hao pia wamesema ongezeko la joto huweza kusababisha kiasi cha umakini kupungua hasa katika kazi kutokana na matumizi makubwa ya chumvichumvi mwilini.

Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti jana ,Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dk. Elisha Osati alisema madhara ya joto yanaweza kusababisha seli za mwili kushindwa kufanya kazi.

“Inapotokea joto mabadiliko yanatokea kwenye mwili kwani wakati huo mwili unapoteza maji na chumvichumvi nyingi na baada ya hapo madhara ni kama ngozi kukauka, figo kushindwa kufanya kazi hivyo mtu anaweza kupata degedege, vipele, majipu wakati mwingine kuishiwa nguvu na hata kupata maambukizi.

“Tuache au kupunguza  pombe kwani zinaongeza kiwango cha joto mwilini kutokana na kemikali nyingi ambazo huweza kupunguza chumvichumvi pia matumizi ya mafuta ya mgando ya kupaka na hata vyakula vya mafuta watu wapunguze,” alisema Dk. Osati.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dk. Longopa George alisema joto linapokuwa juu mapigo ya moyo huongezeka hivyo kusababishao la kazi za  moyo na kusababisha hatari.

“Kuna uhusianao mkubwa kati ya magonjwa ya moyo na joto mapigo ya moyo yanapoongezeka damu nyingi husukumwa mwilini hivyo kufanya mwili kutoa jasho wakati mwingine ukifanya kazi sana unazidiwa na mtu anaweza akapata ‘heart stroke’ hivyo mazingira ya joto ni hatari kwa moyo.

“Mabadiliko yanayotokea ni mtu kuweza kupata kizunguzungu, kichefuchefu, kupoteza fahamu au hata kuchanganyikiwa hayo ni madhara ya joto kwa mwili,”alieleza Dk. George.

Aliwashauri watu kupunguza kiwango cha mazoezi, kukaa kwenye mazingira yasiyo na joto kali na uvaaji wa nguo zisizoakisi joto.

“Kama hakuna ulazima wa kufanya mazoezi usifanye au unaweza kupunguza kiwango cha mazoezi, vinywaji kama pombe na kahawa ni hatari kwa kipindi cha joto na hili la mazingira lizingatiwe kuwe na AC au feni au hata mazingira wazi yenye upepo wa kutosha,”alishauri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles