29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

MADAKTARI WAONDOA UVIMBE KWENYE UBONGO

MUMBAI, INDIA

MWANAMUME mmoja mwenye umri wa miaka 31 nchini India ametolewa uvimbe wa kilo 1.8 na timu ya madaktari nchini humo, baada ya kumfanyia upasuaji mkubwa na wa kipekee wenye lengo la kuondoa uvimbe huo.

Tukio hilo limetokea huko Magharibi mwa Mumbai, baada ya madaktari kumfanyia upasuaji  Santlal Pal, aliyekuwa na tatizo hilo kwa muda mrefu.

Madaktari wanasema uvimbe huo huenda ukawa uvimbe mkubwa zaidi kuwahi kutolewa kwenye ubongo wa binadamu.

Upasuaji huo ulifanyika mnamo Februari 14 na kudumu kwa saa saba, katika hospitali ya Nair mjini Mumbai, magharibi mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Utangazaji la Uingereza (BBC), awali zoezi la upasuaji huo halikutangazwa moja kwa moja, kwa sababu madaktari hawakuwa na uhakika iwapo litafanikiwa na mgonjwa huyo kuwa hai.

“Sasa ni suala la kupona tu, lakini maisha yake hayamo hatarini tena,” alisema Dk. Trimurti Nadkarni, ambaye aliongoza timu ya upasuaji wa mfumo wa neva.

Santlal Pal, muuza duka kutoka Jimbo la Uttar Pradesh, kaskazini mwa India, amekuwa akiishi na uvimbe huo kwa miaka mitatu.

Madaktari wanasema Santal Pal alipoteza uwezo wake wa kuona kutokana na uvimbe huo. Hata hivyo, kuna matumaini kwamba huenda akapata uwezo wa kuona tena baada ya kupona.

Mke wake ameliambia gazeti moja India kwamba aliwahi kuambiwa na madaktari katika hospitali tatu tofauti zilizopo Jimbo la Uttar Pradesh kwamba uvimbe huo hauwezi kuondolewa.

“Matatizo kama hayo huwa hatari sana. Santal Pal alihitaji gramu 11 za damu wakati wa upasuaji huo,” alisema daktari huyo.

Aidha, alitumia mtambo wa kumsaidia kupumua kwa siku kadha baada ya upasuaji huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles