24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Madaktari wanaosomeshwa na Serikali kupangwa vituo vya umma

Na RAMADHAN HASSAN

-DODOMA

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imesema madakatari wote waliosoma kwa fedha za Serikali watapangwa katika vituo vya kazi na serikali.

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Dk. Faustine Ndugulile, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Nanyamba Abdalah Chikota (CCM).

Katika swali lake Chikota alitaka kujua mpango wa muda mfupi wa Serikali wa kupeleka madaktari bingwa katika Hospitali ya Mkoa ya Ligula (Mtwara).

Alisema kwa sasa kuna madaktari ambao wanasoma katika chuo cha MUHAS.

Alisema mara watakapomaliza masomo yao, watapangwa na Serikali kule ambako kuna mahitaji ya madaktari hao.

Dk. Ndugulile alisema wakati huu wa mpito wakiwa wanasubiri kupeleka madaktari hao walio masomoni, Serikali na Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) wamekuwa wakiweka kambi mbalimbali wakiwa na madaktari bingwa ili kutoa huduma za kibingwa.

Akijibu swali la msingi la Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia (CCM), Dk. Ndugulile alisema wizara imefanya tathimini ya mahitaji ya madaktari bingwa na fani zao katika hospitali zote za mikoa, kanda maalum na Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Alisema tathmini hiyo itawezesha utekelezaji wa uamuzi wa kuwapanga upya madaktari bingwa kwa uwiano kulingana na mahitaji ya kila hospitali hizo.

“Lengo ni kuwa kila hospitali hizi zinakuwa na madaktari bingwa wa fani nane. Fani hizo ni pamoja na daktari bingwa magonjwa ya uzazi na wanawake, watoto, magonjwa ya ndani, upasuaji, upasuaji wa mifupa, daktari wa huduma za dharura na magonjwa ya ajali,” alisema 

Pia alisema madaktari wengine bingwa wanaohitajika katika hospitali hizo ni pamoja na daktari bingwa wa huduma za usingizi na daktari bingwa wa huduma ya radiolojia .

Dk. Ndugulile alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2017/18 wizara iliwapeleka madaktari bingwa wa fani za upasuaji wa kawaida na upasuaji wa mifupa 125 katika Chuo cha MUHAS.

Alisema madaktari hao wanatarajia kumaliza masomo yao katika mwaka wa fedha wa 2020/21.

Katika swali lake, Ghasia alitaka kujua nini mikakati ya Serikali katika kupeleka madaktari bingwa katika hospitali ya Ligula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles