Katika mazingira yakutatanisha, madaktari nchini India katika mji wa Amristar wamefanikiwa kutoa visu 40 kutoka kwenye tumbo la mtu wakati wa upasuaji.
Mwanamume huyo (42), alimeza visu hivyo 40 ndani ya miezi mitatu, huku ikiwa bado haijafahamika kusudi lake lilikuwa nini.
Kwa mujibu wa Daktari Jatinder Malholtra, mwanamume huyo hakuwa amewaeleza madaktari juu ya tatizo lake.
“Baada ya vipimo, tuliligundua hilo na ndio tukafanya upasuaji japo ulikuwa ni upasuaji wa aina yake,” alisema Dk. Malholtra
Dk. Malholtra anasema, upasuaji huo ulifanywa na madaktari wapatao watano, ulifanyika kwa takribani saa tano na mgonjwa sasa yupo salama.
“Bado yuko chini ya uangalizi na pia tunatafuta sababu ya kumeza visu hivyo lakini tunaamini kwa kiasi kikubwa kuwa hili ni swala zima linalohusika na matatizo ya kisaikolojia. Na cha ajabu zaidi hata familia yake hawakulikulifahamu jambo hilo,” alisema Dk. Malholtra