27.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, August 17, 2022

MADAI MAPYA YAIBULIWA DHIDI YA MTUHUMIWA WA SHAMBULIZI LA CHRISTCHURCH

Ripoti mpya iliyotolewa na idara ya uchunguzi ya jeshi la polisi la Ujerumani, BKA kuhusiana na shambulizi la misikiti katika mji wa Christchurch nchini New Zealand mwezi uliopita, imesema raia wa Australia anayedaiwa kuwaua takriban watu 50 kwenye shambulizi hilo, mwishoni mwa mwaka 2017 alilitumia kiasi cha dola 2,490 Vuguvugu la siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ufaransa na linalopinga uhamiaji.

Vyanzo vya karibu na kamati ya masuala ya ndani ya bunge la Ujerumani, Bundestag vimeviambia baadhi ya vyombo vya habari kuhusu malipo hayo.

Afisa wa polisi wa BKA amewaambia wabunge kwamba mtuhumiwa alilitumia kundi hilo fedha, kati ya Septemba 18 na 25 mwaka 2017.

Jumatatu iliyopita, mtuhumiwa huyo ambaye ni kiongozi wa kundi la siasa kali za mrengo wa kulia nchini Australia Martin Sellner, alisema kwenye ukanda wa video kwamba alipokea kiasi cha Euro 1,500 mapema mwaka jana, lakini alikana kuhusika na shambulizi hilo la Christchurch.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,894FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles