26.9 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Madagascar yaomba msaada kukabiliana na corona

ANTANANARIVO, MADAGASCAR

WIZARA ya Afya nchini Madagascar, imetuma ombi la msaada wa dharura kwa mashirika na taasisi za Afya huku wagonjwa wa corona wakiongezeka.

Wizara ya Afya imesema kwamba ugonjwa huo katika wiki za hivi karibuni umesambaa kwa kiwango cha juu nchini Madagascar huku maeneo kadhaa yakirekodi milipuko hususan mji mkuu wa Antananrivo, kulingana na mtandao wa Actu Orange.

Kumekuwa na ripoti kwamba hospitali za umma nchini Madagascar zimejaa na zimekuwa zikiwalaza wagonjwa walio katika hali mbaya zaidi.Taifa hilo kwa sasa lina takriban wagonjwa 7,000 wa Covid-19.

Rais Andry Rajaolina mapema mwezi huu aliweka masharti ya kutotoka nje katika mji mkuu wa Antananarivo kufuatia kuongezeka kwa maradhi hayo.

Mnamo mwezi Aprili, alizindua dawa ya mitishamba ya maradhi ya Covid-19 ambayo ilisambazwa nchini humo.

Mizigo kadhaa ya dawa hiyo ya Covid Organic pia ilitumwa kwa makumi ya mataifa barani Afrika.

Hatahivyo uwezo wa kinywaji hicho umepuuziliwa mbali na wataalam wa Afya nchini Nigeria na DR Congo mataifa ambayo yalifanyia majaribio dawa hiyo.

Katikati ya mwezi Julai rais wa taifa hilo alitangaza kwamba wabunge wawili wamefariki kutokana na virusi vya corona huku wabunge wengine 25 wakiambukizwa virusi hivyo tangu kisa cha kwanza kilipothibitishwa katika kisiwa hicho mnamo mwezi Machi.

Rajoleina pia alisema kwamba yeye na familia yake wamekuwa wakinywa dawa ya mitishamba ya Covid Organics inayodaiwa kutibu virusi hivyo ambayo ilizinduliwa mwezi Aprili, licha ya onyo kutoka kwa WHO kwamba haijaidhinishwa kutumika.

“Ni kweli kwamba nimewasiliana na walioambukizwa . Nimeingia katika mahospitali yanayowatibu wagonjwa wa corona. Niko salama.

“Sina virusi vya corona hata kidogo. Sina dalili. Namshukuru Mungu. Nafuata maagizo niliyojiwekea, lakini zaidi ya yote mimi na wapenzi wangu mke wangu na watoto wangu, tunakunywa na kufuata maagizo ya dawa yetu ya mitishamba,” alisema.

BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles