24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Machali ahimiza jamii kutunza miti Bukoba

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera, Moses Machali ameitaka Idara ya mazingira wilayani humo, kutengeneza ratiba na wenyeviti wa mitaa na vijiji itakayohamasisha wananchi kutunza miti inayopandwa karibu na makazi yao.

Machali ametoa kauli hiyo jana kwenye uwanja wa Mashujaa mjini Bukoba wakati akifanya mwendelezo wa upandaji miti aina ya mitende, zoezi ambalo lilizinduliwa na Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango,Machi 8, mwaka huu.

Amesema inashangaza na ni aibu kuona miti iliyopandwa na Serikali karibu na makazi ya Wananchi inakosa afya na kukauka.

“Ni aibu, watu wamekuja kukupandia mti nyumbani kwako wewe, unashindwa hata kwenda kumwagilia maji walau kwa siku moja au wiki, hivyo niwaagize idara ta mazingira kutengeneza utaratibu wa ratiba itakayohamasisha utunzaji miti,”amesema Machali.

Ameongeza kiuwa miti inayopandwa kwenye mazingira yanayokaliwa na wananchi lazima imwagiliwe maji kama ishara ya kukubali kuitunza.

Aidha, amesema mji wa Bukoba unahitaji kupendeza na kuvutia wageni waje kutembelea mandhari safi kwani tayari wazawa walishaanza kuweka mipango yao.

“Hii miti inatokana na wazawa wa mkoa huu, ambao ni watanzania wenzetu wanaishi ndani na nje ya nchi wakiongozwa na Justine Kimodoi kama mwanzilishi wa kampeni,” amesema Machali.

Ameongeza kuwa utunzaji wa miti hiyo utaleta thamani ya mazingira na uhifadhi kwa ujumla kwa kuzingati ushiriki wa wananchi

Afisa Mazimgira Manispaa ya Bukoba, Joseph Tambuko amesema mitende inafaida katika kutunza mazingira na kuepusha mmomonyoko wa ardhi.

“Hii miti aina ya mitende ni rafiki wa mazingira ikilinganishwa na Bukoba kuwa na mvua za mara kwa mara, lakini kubwa ni kwamba ikishapandwa na kukua inatumiwa kama vivutio,”amesema Tambuko

Upande wake Mratibu wa upandaji miti aina ya mitende, Thabith Karwani, amesema lengo nikutaka mji ufanane na miji mingine katika mikoa kwa kuwa na mwonekano mzuri.

Ameongeza kuwa zoezi hilo litafikia wilaya nyingine baada ya kukamilisha kupanda miti 15,000 ya awali kwenye barabara za mji wa Bukoba

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles