27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mabula awataka vijana kujifunza kwa Nyerere

Mwandishi wetu -Butiama

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk. Angeline Mabula, amewataka vijana kujifunza maisha ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa vitendo ili matendo ya kiongozi huyo wa kwanza wa Tanzania yaendelee kukumbukwa.

Akiwa katika maadhimisho ya miaka 20 ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria, Jimbo la Musoma, Parokia ya Butiama mkoani Mara jana, Dk. Mabula alisema ni vyema vijana wakatumia hazina ya wazee kama Mwalimu Nyerere kuwa chachu ya kuishi kwa vitendo.

“Niwaombe vijana kutumia hazina ya wazee wetu na kuwa chachu ya kuishi kwa vitendo,” alisema.

Dk. Mabula ambaye alikuwa mkuu wa kwanza wa Wilaya ya Butiama, alihitimisha salamu zake za miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere kwa kuwataka wananchi kuishi pia kwa kumcha Mungu kwa kuwa wakati wa uhai wake Baba wa Taifa aliishi kwa kumcha Mungu.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba, alimwelezea Mwalimu Nyerere kuwa alikuwa ni mtu wa maisha ya Mungu aliyejitahidi kujenga umoja na mshikamano kwa nchi yake na Afrika kwa ujumla.

Naye Makamu Mwenyekiti wa CCM, Phillip Mangula, alimwelezea Mwalimu Nyerere kama mtu aliyepigania haki na aliyesisitiza kuwa binadamu wote ni ndugu na Afrika ni moja.

Maadhimisho hayo yalihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,  Steven Wasira na Mbunge wa Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles