22 C
Dar es Salaam
Sunday, June 4, 2023

Contact us: [email protected]

Mabondia watambiana kung’oana meno Kinesi

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

JUMLA ya mapambano 14 ya ngumi za kulipwa yanatarajia kupigwa Jumamosi Julai 17, 2021 kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar es Salaam, huku kila bondia akitamba kumaliza pambano kwa K.O.

Katika mtanange huo, moja ya pambano la kisasi, litamkutanisha Ibrahim Tamba na Hussein Itaba.
Mabondia wengine ni Ally Gonja, atapigana na Omary Mpemba, Abdul Ubaya dhidi ya Pius Simon, Jesca Mfinanga atazitwanga na Dorothea Muhoza.

Akizungumza wakati wa utambulisho wa wanamasumbwi hao, promota wa mapambano hayo, Selemani Semunyu, amesema michezo hiyo ni maandalizi ya kuelekea pambano kubwa linalowakutanisha Twaha Kiduku na Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,284FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles