27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mabomba mabovu yakwamisha mradi wa maji Kayenze

Naye  Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire.
Naye Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire.

Na Peter Fabian, MWANZA

MIRADI miwili ya majisafi inayosimamiwa na Halmashauri ya Jiji la Mwanza  imeshindwa kukamilika kwa muda mrefu sasa kutokana na ubovu wa mabomba na viunganishi vyake, imefahamika.

Habari zinasema hali hiyo imekuwa ni mateso kwa wananchi wa Kata ya  Kayenze wilayani Ilemela  na Fumagila, Kata ya Kishiri Wilaya ya Nyamagana, ikizingatiwa imegharimu zaidi ya  Sh bilioni 1.6.

“Katika mradi wa Kayenze vifaa  viko chini ya kiwango na taarifa zinaonyesha   fedha iliyotumika kununulia vifaa hivyo ni zaidi ya Sh milioni 800.

“Vilevile   mkandarasi wa kazi hii hajulikani lakini Halmashauri ya Jiji la Mwanza ndiyo msimamizi.

“Mradi   ulianza   mwaka 2011 hadi leo ni miaka mitano   majisafi hayajatoka kwa wananchi hili ni jipu,” kilieleza chanzo chetu za habari.

Alisema kwa mradi wa Fumagila-Kishiri (Nyamagana)   wataalamu   wamekuwa wakidai uko kwenye majaribio ya mwisho ili kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Hata hivyo, alisema tatizo ni lilelile la    ununuzi wa vifaa vilivyo chini ya kiwango vya thamani zaidi ya Sh milioni 700 kiasi kushindwa kutoa maji.

Mbunge wa   Nyamagana, Stanslaus Mabula (CCM) amekuwa akiwaomba wataalamu wa halmashauri kukamilisha mradi huo bila mafanikio.

“Fedha ya serikali iliyotolewa na Wizara ya Maji imetafunwa kwa kununuliwa vifaa vilivyo chini ya kiwango…  maji  yakifunguliwa maji tu mabomba yote yanapasuka,” alisema Mbunge huyo.

Baadhi ya wananchi wa   Fumagila wametaka hatua kali zichukuliwe kwa wataalamu wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutokana na mradi huo   kushindwa kutoa huduma kwa muda mrefu.

Naye  Meya wa Jiji la Mwanza, James Bwire   amemtaka Mkurugenzi wa Jiji hilo, Kiomoni Kibamba kuhakikisha mradi huo unakamilika na kuanza kutoa huduma kwa kuwa fedha zilikwisha kutolewa na Wizara ya Maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles