29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

Mabingwa 50 kushuhudia Derby ya Kariakoo kwa Mkapa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

KAMPENI kubwa ya Mtoko wa Kibingwa yazinduliwa rasmi huku mabingwa 50 kushuhudia Derby ya Kariakoo iatakayozikutanisha miamba ya Soka nchini Simba na Yanga, katika Jukwaa la VIP A Novemba 05,2033 Kwa Mkapa.

Afisa Habari wa Kampuni ya Betika, Juvenalius Rugambwa akizungumza na Wanahabari leo Oktoba 02,2023 jijini Dar es Salaam wakati akizindua Promosheni ya Mtoko wa Kibingwa msimu wa 06 ambao utamalizika mwisho mwa mwezi oktoba mwaka huu ikijumuisha washindi 50 watakaojishindia tiketi za ndege na VIP A kushuhudia derby ya Kariakoo Novemba mwaka huu

Akizungumza na Wanahabari leo Jumatatu Oktoba 02, 2023 Afisa Habari wa Kampuni ya Betika, Juvenalius Rugambwa amesema kampuni hiyo imekuwa karibu na wateja wake kwa promosheni mbalimbali ili kuonesha jinsi gani ina wajali na wanamichezo kwa ujumla na kufikisha wateja 300 wa promosheni ya Mtoko wa Kibingwa msimu uliopita.

Rugambwa ameeleza kuwa promosheni ya mtoko wa kibingwa msimu wa 06 utakuwa wa kitofauti zaidi ambapo washiriki 50 watapata huduma za malazi ,usafiri pamoja tiketi ya VIP A kwa ajili ya kushuhudia derby hiyo huku zaidi mengine yakibaki kuwa ya Surprise ili kuleta utofauti kwa mabingwa wa msimu uliopita.

Aidha, amefafanua zaidi kupitia promosheni hiyo imekuwa na muitikio mkubwa sana kutokana na washiriki wengi kutokea mikoani.

“Kama Betika tunapata muitikio mkubw wakuendelea kuwepo kwa promosheni hii kutokana na washindi wengi kutokea mikoani hivyo tunapata muitikio kuwa kampuni imefika mbali zaidi na huduma zinawafikia tunapata mrejesho mzuri wa kampuni yetu kujitangaza,” amesema.

Pia amesema mabingwa wa promosheni hiyo watapatikana kwa njia ya droo ambazo zitafanyika kila wiki siku ya Jumanne ambapo rasmi zitaanza Oktoba 10,2023 na kufikia kilele chake Oktoba 31,2023.

“Ni rahisi mshiriki anatakiwa kuwa na vigezo vya kushirikiambavyo ni kubeti mkeka wenye mechi kuanzia 3 na dau la kubeti liwe kuanzia Sh 2,000 au zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles