23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mabalozi waipa tano Zara Tours, waahidi makubwa

Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Mabalozi 11 wanaowakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali Duniani waimwangia sifa kampuni ya Zara Tours Adventures Tanzania, kwa kutoa huduma bora kwa wageni waliopanda mlima Kilimanjaro kupitia kanpeni ya Twende zetu kileleni iliyoenda sambamlba na maadhimisho ya miaka 62 ya Uhuru wa Tanganyika.

Ikumbukwe kuwa kupitia kanpeni ya mwaka huu zaidi ya watu 220 walipanda mlima Kililanjao ambapo njia tatu zilitumika.

Akizugumza mara baada ya kushuka mlima Kilimanjaro Amidi wa muda wa mabalozi hao, Balozi Maadhi Maalim amesema kampuni ya Zara ni miongoni mwa kampuni bora za wazawa inayosimamiwa na Mwanamke.

Amesema kampuni hiyo imejikita zaidi katika kuhakikisha kuwa wanawalea wageni waofika kutalii nchini kama watoto wadogo huku wakifanya kazi kwa ushirikiano na kwamba inapaswa kuwa mfano wa kuiogwa na kampuni nyuingine zilizowekeza katika sekta ya utalii ili kuleta mageuzi makubwa.

“Mama Zainab Ansell ni mmoja wadau wa utalii ambao wamejipanga kutoa huduma kwani muda wote watu wake wamekuwa wakifanya kazi kwa moyo, upendo na furaha kwa siku sita tuliopanda mlima tulifurahia kwani tulipata ushirikiano wa kutosha na kufanya tuifurahie safari yetu,” amesema Balozi Maalim.

Ameo,geza kuwa wao kama mabalozi watakwenda kuitangaza Zara kama mchango wao kwa Mama Zara Tours, kutokana na kuonyesha uzalendo katika kuunga mkono jitihada za Serikali inayoongozwa na Dk. Samia Suluhu Hassan katika kunyanyua sekta ya utalii.

Naye Balozi Humphrey Polepole nchini Cuba amempongeza Rais Dk. Samia kwa kuwapatia kibali cha kushiriki kampeni ya Twende zetu kileleni kupandisha bendera katika kilele cha mlima Kilimanjaro kuadhimisha miaka 62 ya uhuru wa Tanganyika.

Amesema wao kama mabalozi watakwenda kufanya jukumu la kumuunga mkono rais katika nchi wanazowakilisha ili kuleta watalii wengi zaidi nchini.

“Tunampongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hasan kutupa ruhusa kuja kushiriki zoezi hili ni jambo la furaha sana hili inaonyesha dhahiri kwamba sisi kama mabalozi hatuna budi kwenda kutangaza vivutio vyetu vya utalii na kuleta wengi zaidi, Rais anafanya kazi kubwa katika kuiletea maendeleo nchi yetu,” amesema polepole.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Zara Tours, Zainab Ansell amesema wameendelea kuboresha hudumu ikiwa ni pamoja na kutoa fursa za watalii wa ndani ambapo wameweka kiwango cha Sh 1,500,000 kupanda mlima Kilimanjaro.

Amesema kuwa ni rahisi kwa wananchi kulipa kwani wanaweza kulipa kidogo kidogo.

Amesema kampuni hiyo pia imeanzisha kampeni mpya ya Twende zetu Serengeti ambayo wanatarajiwa kuanza rasmi mwanzo mwa mwaka 2024, lengo likiwa nikuhamishisha utalii wa ndani nakuunga jitihada za serikali katika kukuza utalii na kuongeza pato la Taifa kupitia utalii ikiwamo kuchochea ajira.

Upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki amesema mlima Kilimanjaro unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi, kukauka kwa baadhi ya vyanzo vya maji.

Aidha, Waziri Kairuki ametoa wito kwa wananchi kutovamia maeneo ya uhifadhi na kuacha tabia ya kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya maeneo ya hifadhi.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki.

Waziri Kairuki amesema serikali imeweka lengo la kufikia watalii milioni 5 watakaoliingizia Taifa dola za Kimarekani Bilioni 6 ifikapo mwaka 2025, ambapo ili kufikia lengo hilo TANAPA hawana budi kuainisha, kuongeza na kuboresha vivutio vilivyopo nchini ili kuvutia watalii wengi zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles