28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Mabaki yaliyopatikana Pemba ni ya ndege iliyotoweka Malaysia

Waziri wa Uchukuzi wa Malaysia, Liow Tiong Lai.
Waziri wa Uchukuzi wa Malaysia, Liow Tiong Lai.

KUALA LUMPUR, MALAYSIA

SERIKALI ya Malaysia imethibitisha kuwa mabaki ya ndege yaliyookotwa katika pwani ya Kisiwa cha Pemba nchini Tanzania, ni ya ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia iliyotoweka Machi 2014.

Waziri wa Uchukuzi wa Malaysia, Liow Tiong Lai, ameripotiwa akisema jana kuwa baada ya uchunguzi, imebainika kipande hicho kikubwa cha bati kilichopatikana Juni ni cha ndege hiyo chapa MH370.

Alisema uamuzi huo ulifikiwa kwa pamoja na wataalamu kutoka Idara ya Usalama wa Safari za Ndege ya Australia (ATSB) na wale wa kikosi maalumu cha kuchunguza usalama wa MH370.

Mapema Julai, Waziri wa Uchukuzi wa Australia, Darren Chester, alikuwa amedokeza kuwa kulikuwa na uwezekano mkubwa mabaki hayo yalikuwa ya ndege hiyo.

“Ni kutokana na muundo wa mabaki hayo, ukubwa wake na muonekano wake,” alisema.

Mabaki hayo pia yalikuwa na muhuri wa kuonyesha tarehe ya kuundwa kwake – Januari 23, 2002.

Kwa mujibu wa tovuti ya shirika la habari la Channel Asia, ndege hiyo ya Malaysia ilikabidhiwa kwa shirika hilo Mei 31, 2002.

Ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilitoweka Machi 2014, ikiwa na abiria 239 baada ya kuruka kutoka Malaysia kuelekea Beijing, China.

Liow alisema mabaki hayo yatachunguzwa zaidi kubaini iwapo kutapatikana ufumbuzi kuhusu kilichotokea hadi ndege hiyo ikatoweka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,455FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles