30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

Mabadiliko ya sheria yatasaidia vyombo vya habari kiuchumi- Wakili Marenga

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Kwa nyakati tofauti wadau mbalimbali wa tasnia ya habari nchini wamekuwa wakipambana kuhakikisha kuwa Serikali inafanya mabadiliko ya baadhi ya vifungu katika Sheria ya Huduma za Habari (Media Services Act) ya mwaka 2016.

Kama inavyofahamika kwamba katika sheria hiyo kumekuwa na baadhi ya vifungu ambavyo ni ‘mwiba’ kwa tasnia ya habari nchini.

Ikumbukwe kuwa sheria hii ilipitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 5, mwaka 2016 na kutiwa saini na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dk. John Magufuli Novemba 16, 2016 nakuanza kutumika rasmi.

Akizungumza na Mtanzania Digital Septemba 22, mwaka huu, James Marenga ambaye ni Wakili wa Kujitegemea na Makamu Mwenyekiti wa MISA–TAN anasema kuwa kuna baadhi ya vifungu ambavyo iwapo vitaendelea kutumika basi vitakuwa vinabana ustawi wa vyombo vya habari na wanahabari wenyewe kwa ujumla.

Wakili James Marenga.

Changamoto ya kifungu hicho ni kwamba Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ndiye mshauri mkuu wa serikali kwenye masuala ya habari, uchapishaji na utendaji wa vyombo vya habari.

Akitaja moja ya vifungu hivyo, Wakili Marenga anasema kuwa ni kile cha 5 (1) ambacho kinatoa mamlaka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo kuratibu matangazo yote yanayotoka serikalini.

“Kumpatia mamlaka ya kuratibu masuala ya matangazo anaweza kuwa na upendeleo na kunyima matangazo kwenye magazeti ambayo yataonekana kuchapisha habari ambazo zina mtazamo tofauti na serikali.

“Hivyo, hii itafifisha uchipukaji wa mawazo anuwai katika jamii na kukwaza uhuru wa kujieleza. Tunapendekeza kufutwa kwa kifungu hiki kwani kutatoa nafasi kwa taasisi za umma kutoa matangazo yao kwa magazeti wanayoona yanafaa kwao na yenye kufika sehemu kubwa ya nchi. Pia vyombo vya habari binafsi vitanufaika na matangazo hayo.

“Lakini pia itaathiri uchumi wa vyombo vingi vya habari kwani vitakuwa vinjiendesha katika mazingira magumu hatua itakayodhoofisha hata uchumi wa wanahabari wenyewe,hivyo ndiyosababu tunapigia kelele serikali iweze kubadilisha kifungu hiki,” amesema Wakili Marenga.

Kwa muda mrefu sasa wadau wa tasnia ya habari nchini wanaendelea na hatua mbalimbali za kuhakikisha kuwa mabadiliko ya sheria yanafanyika hatua itakayoleta ustawi wa taaluma hiyo muhimu nchini.

Hata hivyo, kuanza kuonekana dalili njema za serikali kutaka kufanyia kazi mapendekezo hayo ya wadau ambapo kama ambavyo wamekuwa wakinukuliwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

Akifungua Mkutano wa Wadau wa Maendeleo Julai 13, mwaka huu jijini Dar es Salaam Waziri Nape alisema kuwa serikali imepokea maoni nayo ikatoa yakwake juu ya kuboresha tasnia ya habari.

“Kwa hapa tulipofika wadau wana furaha, hata ukiwaita na ukiwauliza. Wameleta maoni yao nasi tumetoa ya kwetu, tumejadiliana ili kuona namna ya kuboresha.

“Sheri ya Habari ilipotungwa, ililenga kutatua matatizo ya habari ikiwemo matatizo ya ajira zao, maslahi yao, mazingira yao ya kazi, haki zao na wajibu wao. Sasa inawezekana masuluhisho yaliyopo kwenye sheria, ndio yanayogombaniwa kwamba ni sahihi ama si sahihi,” amesema Waziri Nape na kuongeza kuwa.

“Katika mazingira hayo, serikali imetoa nafasi kwa wanahabari kuleta mbadala wa yale yanayolalamikiwa, tukae mezani tuzungumze na huo mchakato haiwezi kuwa mfupi, ni chakato wa mazungumzo mie nimeukuta na tuaendelea nao. Tuna malengo ya kuukamilisha mapema kadri inavyowezekana.

“Lengo tutunge sheria itakayokaa muda mrefu lakini sheria itakayokubalika na pande zote mbili lakini itakayotengeneza mazingira kuwa bora zaidi kuliko tuliyonayo,” amesema Nape

Kama hiyo haitoshi katika kuzidndea dalili hizo njema, Septemba 20, Mwaka huu Msemaji Mkuu Msigwa abainisha kuwa mchakato wa marekebisho ya sheria zinazosimamia sekta ya habari nchini umefika hatua nzuri.

Msigwa alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa alipoulizwa juu ya hatua iliyofikiwa baada ya kikao cha wadau wa habari na serikali cha Agosti 11 na 12, mwaka huu.

Mkurugenzi wa Idara ya Habari-(MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa.

Akijibu swali hilo kwa ufupi, Msigwa alisema mchakato wa mabadiliko ya sheria ya habari unaendelea na upo katika hatua nzuri ndani ya serikali.

“Subirini, muwe na Subira mtajulishwa hatua lakini mpaka sasa mchakato unakwenda vizuri,” amesema Msigwa na kusisitiza kwamba, serikali itatoa taarifa ya hatua zinazoendelea,” alisema Msigwa.

Septemba 21, mwaka huu akizungumzia mchakato huo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, amesema ingawa mpaka sasa hajajua wakati ambao mapendekezo hayo yatafikishwa bungeni, lakini bado ana matumaini kwamba safari ya mabadiliko hayo haitaishia njiani.

Balile amesema, serikali bado inaonesha kuwa na dhamira njema ya kufanya mabadiliko.

“Waziri wa Habari ndiye mwenye kujua lini watapeleka bungeni muswada lakini sisi wadau tumepewa fursa ya kutoa maoni yetu.

“Tumeona dhamira njema ya serikali hadi hivi sasa, tukiendelea hivi nadhani huko tuendako tutashirikiana vizuri kwa masilahi ya Taifa letu,” amesema Balile.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile.

Mchakato wa mabadiliko ya sheria zinazominya uhuru wa habari nchini, ulishika kasi baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza serikali na wadau kukaa Pamoja na kuangalia namna ya kumaliza kero hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles