28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mabadiliko ya sheria ya sukari yatawakomboa Watanzania

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kufuatia upotoshaji unaoendelea kutolewa na baadhi ya watu wasiokuwa na ufahamu juu ya sheria mpya ya sukari, Bodi ya Sukari Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu mabadiliko hayo.

Bodi imeeleza kuwa sheria hiyo mpya, iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inalenga kudhibiti mfumuko wa bei ya sukari ili isimuumize mwananchi, kuhakikisha upatikanaji wa uhakika, uwazi katika usambazaji wake, pamoja na ufanisi kwenye viwanda vya sukari nchini.

Hayo yamesemwa leo Julai 5, 2024, na Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania, Profesa Kenneth Bengesi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Ufafanuzi huo umekuja baada ya baadhi ya wadau wa sekta ya sukari kuelezea sakata hilo bila kuwa na taarifa za kutosha, hali iliyoibua sintofahamu kwenye sekta hiyo nyeti nchini.

“Baadhi ya watu wanaoelezea suala la sukari hawana taarifa za kutosha, hivyo ni jukumu letu kama Bodi kutoa picha kamili ya namna gani Watanzania watafaidika na mabadiliko haya katika sheria ya sukari,” amesema Profesa Bengesi.

Profesa Bengesi ameendelea kufafanua kuwa baadhi ya hoja zilizofafanuliwa na Bodi ya Sukari Tanzania ni pamoja na uhaba wa sukari, malalamiko ya utoaji wa vibali, na mbinu zinazotumika kuhakikisha uhaba wa sukari nchini unaisha.

“Serikali imefanya mabadiliko haya kwa nia ya kuleta ahueni kwa wananchi na kuleta ufanisi katika sekta ya sukari. Tunawahakikishia wananchi kuwa mabadiliko haya yatasaidia kupunguza changamoto zilizopo na kuleta maendeleo endelevu katika sekta hii muhimu,” ameongeza Profesa Bengesi.

Kwa mujibu wa Profesa Bengesi, Bodi ya Sukari Tanzania itaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu sheria mpya ya sukari na mafanikio yanayotarajiwa kutokana na utekelezaji wake. Amewataka wananchi na wadau wa sekta ya sukari kuwa na subira na kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles