23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Maaskofu Katoliki wawagomea mashoga

VaticanVATICAN CITY, VATICAN

MAASKOFU wa Kanisa la Katoliki juzi waligoma kupitisha mabadiliko makubwa ya kihistoria kuhusu msimamo wao mkali dhidi ya masuala ya ushoga, utoaji mimba na wanandoa waliotalikiana.

Uamuzi huo,ulifichua uwapo wa pengo kubwa ndani ya kanisa hilo mwishoni wa mkutano huo wa wiki mbili.

Maaskofu wa kanisa hilo walikuwa wamekutana kujadili jinsi mafunzo ya kanisa hilo yanavyoweza kufanyiwa mageuzi ili kuambatana na maisha ya kisasa.

Hiyo ni pamoja na kukaribisha ‘zawadi na sifa’ za mashoga Wakatoliki na mwito kwa mapadri kuepuka lugha au tabia yoyote inayoweza kuwanyanyapaa Wakatoliki waliotalikiana.

Wakati lugha kuhusu mashoga ikiwa imelegezwa wakati wa siku za mwisho za majadiliano hayo, waraka wa mwisho uliopendekezwa ulishindwa kupata theluthi mbili ya kura zilizohitajika.

Hata hivyo,maaskofu walisifu upendo wa kweli katika ndoa ya kawaida, wakiita moja ya miujiza mizuri zaidi na inayokubalika.

Kwa kushindwa kukubaliana kwa kauli moja, kunamaanisha kushindwa kwa kauli za kipatanishi za Papa Francis tangu achaguliwe upapa zaidi ya  mwaka mmoja uliopita.

Mwaka jana, Papa Francis aliwafurahisha wanaharakati za ushoga wakati alipoonekana kulegeza msimamo wake.

Alipoulizwa swali iwapo mashoga wanapaswa kuwa Wakristo wazuri, alijibu kwa kuuliza, ‘Mimi ni nani hata nihukumu?

Hata hivyo, baada ya viongozi wa Katoliki kupiga kura hiyo, Papa Francis aliwaonya maaskofu dhidi ya ‘ukali lugha’ wakati wa kujadili masuala tete yanayolikabili kanisa hilo.

Msemaji wa Vatican, Federico Lombardi alipoulizwa kuhusu kilichofikiwa katika mkutano huo, alisema waraka uliopo ni mwongozo kwa maaskofu katika utumishi wao na unaweza kujadiliwa tena mwaka ujao.

“Si muhimu kwenda mbali zaidi kuuchambua. Kifupi ni kwamba maaskofu wa sinodi hawakufikia uamuzi wa mwisho kuhusu waraka huo.”

Hatua ya maaskofu kukataa kufanya mageuzi imepokewa kwa ghadhabu na makundi ya kikatoliki yanayopigania haki za wapenzi wa jinsia moja.

Hata hivyo, kundi la kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja nchini Marekani la New Ways Ministry, limesema hatua ya maskofu hao kuamua kujadili suala hilo ni matumaini ya siku za usoni.

- Advertisement -

Related Articles

4 COMMENTS

  1. Kanisa katoliki haliendeshwi kishabiki kama vtyama vya siasa. Lina msingi imara ambayo haitegemei baba Mtakatifu bali uongozi wa kanisa wakiwamo, makadinali, maaskofu, mapadre, na waumini wote kwa pamoja. Masuala ya Ushoga, utoaji mimba, na mengine msahau kabisa kwamba yatalegezwa hayo yanaambatana na misingi mikubwa sana ya kanisa katoliki. Vyombo vya habari na ushabiki wake vitaendelea kugonga mwamba katika kutaka kuyumbisha kanisa katoliki dunia. Hongereni sana maaskogu wa sinodi nipo pamoja nami.

  2. HAKUNA JIPYA CHINI YA JUA, HUU NI MTEGO MKUBWA, TUSIJETUKAWA MAFARISAYO KWA KUWAFURAHISHA WANADAMU, YALIYO ANDIKWA YANATIMIA. SHIKA SANA ULICHONACHO.

  3. Neno la Mungu (Biblia) ni mwongozo thabiti katika kuamua yapi ya kufanya na yapi sio ya kufanya kupitia hekima iletwayo na Roho Mtakatifu. Ikiwa neno limekataa basi wafuasi (wakristo) walifuatao neno wanapaswa kukataa sawa na neno kwa kuwa waliingia mkataba na kanisa kupitia UBATIZO. Swala la kuleta maisha ya kisasa ndani ya kanisa ni kubatilisha ukweli wa neno la Mungu kwa matumizi ya JANA.LEO NA HATA MILELE.Na wakitaka kuingiza ushoga ndani ya kanisa wanapaswa watengue kwanza mkataba wa ubatizo kisha wajitenge wenyewe pasipo kudai haki yoyote kutoka kanisani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles