Maarifa zaidi yahitajika kupata dawa ya corona

0
986

 CALFONIA, MAREKANI

MAKAMPUNI ya utengenezaji wa dawa za kupambana na ugonjwa wa corona duniani yanakuna kichwa usiku na mchana kukabiliana na janga hilo.

Kampuni ya utengenezaji dawa ya Exscientia, ilikuwa ya kwanza kutoa dawa iliyofikia hatua ya kufanyiwa majaribio kwa binadamu, inafuatilia dawa 15,000 kutoka taasisi ya utafiti ya Scripps, California.

Pia Kampuni ya Cambridge iliyoanzishwa na mvumbuzi mwenza wa dawa ya viagra, Dk. David Brown, imefanya mabadiliko ili kugeukiwa uchunguzi wa kuvumbua wa dawa za magonjwa nadra.

Taarifa zinasema, kawaida mchakato wa utengenezaji dawa mpya umekuwa wa polepole.

“Nimekuwa nikifanya kazi hii kwa miaka 45, nimefanikiwa kutoa dawa tatu ambazo zipo sokoni,” daktari Brown aliiambia BBC News.

“Imechukua wiki kadhaa kupata taarifa tunazohitaji,tumepata taarifa mpya siku chache zilizopita na sasa tuko kwenye kipindi muhimu mnoo.

“Mchakato ulianza sikukuu ya pasaka, tutakuwa na matokeo ya njia hizo tatu siku saba zijazo,”alisema

Kampuni ya Healx, inatarajia taarifa hizo zitawezesha kutengenezwa kwa dawa kadhaa kufikia Mei na tayari inafanya mazungumzo na maabara kadhaa kuchukua matokeo hayo na kuyapeleka kwenye kliniki ili kufanyiwa majaribio.

Kwa waliopo kwenye nyanja ya kutafuta dawa, wana machaguo mawili linapokuja suala la virusi vya corona:

Watalaamu wanasema kutafuta dawa mpya kabisa, itachukua miaka kadha kabla ya kuidhinishwa kuwa salama kwa matumizi ya binadamu

Lakini kulingana na Dk.Brown, ni vigumu kwa dawa moja kuibuka kuwa na uwezo wa kutibu virusi vya ugonjwa huo.

Profesa Ara Darzi, mkurugenzi wa taasisi ya uvumbuzi wa dawa duniani, imeambia BBC kuwa Kampuni ya Healx, ni moja ya zinazotegemewa kupata uvumbuzi wa dawa ya ugonjwa huo, lakini kuna haja ya kuwa na takwimu za kutosha.

“Sasa kuna haja kubwa ya kukusanya pamoja data zote hizo ili kuwezesha upatikanaji wa dawa mpya itakayotibu ugonjwa wa Covid-19 haraka iwezekanavyo,”

Kawaida kuleta makampuni pamoja ili kushirikiana inachukua mwaka mzima”, amesema mkuu wa kampuni ya utengezaji dawa ya Schipher, Alif Saleh.

Alisema kupitia teknolojia kama vile mikutano kwa njia ya video, kumeharakisha mazungumzo kwa makampuni ya kutengenza dawa ya kukabiliana na civid-19.

“Kile ambacho kimefanyika kipindi cha wiki tatu zilizopita, kingefanyika kwa kipindi cha nusu mwaka,” alisema.

Tayari utafiti ambao umefanywa na makampuni hayo umezindua matokeo ya kushangaza: Virusi vya corona vinaweza kuingia kwenye tishu za ubongo na hilo linaelezea kwanini baadhi ya watu wanapoteza hamu ya kula na ukosefu wa uwezo wa kuvuta harufu.

Pia unaweza kuathiri mfumo wa afya ya uzazi kwa wanaume na wanawake.

“Mbinu tofauti tofauti zinatumika kwa mitazamo tofauti lakini zote zina zina uhakika,” alisema Profesa Albert-Laszlo Barabasi.

Kuna baadhi ya kampuni za kutengeneza dawa zinazosema tayari zimegundua dawa ambazo zinaweza kusaidia pakubwa kupata tiba ya virusi vya corona.

Kampuni ya Benevolent, imetambua dawa ya Baricitinib ambayo inatumika kutibu ugonjwa wa baridi yabisi, yaani rheumatoid arthritis kama yenye uwezo wa kutibu na kuzuia maambukizi ya virusi hivyo kwenye seli za mapafu.

Hivi sasa inafanyiwa majaribio na Taasisi ya Taifa ya Marekani ya kukabiliana na magonjwa ya kuambukiza na mzio.

Wakati huohuo, wanasayansi kutoka Korea Kusini na Marekani, wanafanya utafiti wa uwezekano wa dawa za kuzuia maambukizi na kupendekeza dawa ya Atazanavir, inayotumika kudhibiti makali ya Ukimwi, inaweza kuwa dawa nzuri zaidi.

Kampuni ya Teknolojia ya Alibaba, kwa mfano, imetangaza kifaa chenye uwezo wa kubaini ugonjwa huo ndani ya sekunde 20 ambacho usahihi wake ni asilimia 96.

 Kuna haja ya kuimarisha juhudi za kimataifa kuanzia kwa watungaji wa sera, kushawishi makampuni makubwa ya kutengeneza dawa kushirikiana na kampuni ndogo, wanasayansi na mashirika ya utafiti kuleta pamoja raslimali za upatikanaji wa takwimu, alisema Profesa Darzi.

“Hiki ni kipindi muhimu sana cha kupata takwimu za dawa ili kusaidia kukabiliaba na ugonjwa wa Covid-19,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here