28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

Maandamano yaendelea Algeria

ALGIERS, ALGERIA

WAANDAMANAJI nchini Algeria walifurika mitaani kwa wiki ya 13 mfululizo juzi, ambapo waliyaparamia magari ya polisi yaliyoweka kizuizi cha kulifikia eneo maalumu la maandamano katikati ya Mji Mkuu, Algiers. 

Vikosi vya usalama vilifyatua mabomu ya kutoa machozi dhidi ya kundi la waandamanaji katikati ya mji huo, ili kuwazuia kuyafikia makao makuu ya ofisi za posta, lakini waliondoa vizuizi walivyoweka baada ya waandamanaji kupanda juu ya magari. 

Mamia kwa maelfu ya waandamanaji walijitokeza mjini Algiers na kwenye miji mingine kaskazini ya nchi hiyo katika vuguvugu la kusaka demokrasia lililoanza Februari 22 mwaka huu, ambalo lilifanikiwa kuuangusha utawala wa Rais Abdelaziz Bouteflika. 

Hivi sasa waandamanaji wanataka maofisa wa ngazi ya juu, ikiwamo rais wa mpito, Abdelkadir Bensalah kuondoka madarakani ili kupisha enzi mpya kwa Algeria. 

Mkuu wa jeshi, Ahmed Gaid Salah, ambaye pia analengwa na baadhi ya waandamanaji amesisitiza umuhimu wa kufanyika kura ya urais mnamo Julai 4, tarehe iliyowekwa na kiongozi wa mpito ili kuheshimu katiba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles