22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Maandamano ya “Black lives Matter” yafanyika kwa amani Australia

CANBERRA, AUSTRALIA

MAANDAMANO ya kusisitiza umuhimu wa maisha ya watu weusi ’Black Lives matter’, yameendelea kwa amani nchini Australia wakati maelfu ya watu katika mji mkuu Sydney wakiyaenzi maisha ya George Floyd na kukasirishwa na mauaji ya wakaazi wa asili wa Australia chini ya ulinzi wa polisi. 

Waandaaji wa maandamano hayo walipata fursa ya kuandamana katika dakika za mwisho baada ya kukata rufaa ya ombi lao la kutaka kuandamana, ambalo awali lilikataliwa. 

Mahakama ya rufaa ya jimbo la New South Wales ilitoa ruhusa ya kuandamana dakika 12 kabla ya muda wa kuandamana kufika, hii ikimaanisha wale wanaoshiriki hawatokamatwa. 

Jaji wa Mahakama hiyo, Grant Stevens amesema hili ni tukio la aina yake na watu wanapaswa kuwa na haki ya kuandamana kuhusu mambo muhimu. 

Maandamano hayo yalikuwa ya amani huku polisi wakionekana wakitoa barakoa kwa waandamanaji na wengine wakitoa vitakasa mikono. 

Kifo cha George Floyd, Mmarekani mweusi aliyeuwawa akiwa amefungwa pingu wakati polisi mzungu wa mjini Minneapolis, alipogandamiza goti lake katika shingo yake kwa takriban dakika tisa hata baada ya kusema kuwa hawezi kupumua, kimesababisha maandamano kote duniani kupinga ukatili wa polisi na ubaguzi wa rangi.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,502FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles