28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

MAANDAMANO MAKUBWA YA WAPALESTINA YATARAJIWA KUITIKISA MASHARIKI YA KATI

Wapalestina wanajiandaa kuadhimisha matukio mawili muhimu ya kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu yalipoanza maandamano makubwa ya aina yake yaliyofanyika katika mpaka wa Gaza na Israel na siku ya ardhi.

Maandamano ya kumbukumbu hizo yanatowa mwito wa kudai haki ya kurudi kwa wakimbizi wakipalestina katika ardhi zao ambazo kwa sasa zinashikiliwa kwa mabavu na Israel pamoja na kukomeshwa kwa hatua ya mzingiro inayochukuliwa na Israel katika ardhi ya Wapalestina.

Maandamano hayo yanatarajiwa kufikia kilele chake jumamosi,miito ikitolewa ya kuwataka mamilioni ya watu wajitokeze sio tu katika ardhi ya Wapalestina na Israel lakini hata katika nchi za kiarabu na nchi za Ulaya.

Zaidi ya wapalestina 260 waliuwawa na maelfu kujeruhiwa tangu Maandamano makubwa ya kushinikiza haki ya wakimbizi wa kipalestina kurudi katika ardhi yao,yaliyoanza Machi 30 mwaka jana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles