27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Maandalizi kuapishwa JPM yamekamalika

Ramadhani Hassan -Dodoma

SERIKALI imesema maandalizi  ya kupishwa Rais mteule Dk. John Magufuli yamekamilika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini,Msemaji  Mkuu wa Serikali,Dk.Hassan Abassi alisema  Dk. Magufuli ataapishwa Alhamisi  Uwanja wa Jamhuri na kushuhudiwa na  wageni mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi wamethibitisha kushiriki.

“Nitoe taratibu za Serikali,baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kukamilisha taratibu zao, mgombea wa urais kukabidhiwa cheti chake, ataapishwa Uwanja wa Jamhuri hapa Dodoma,”alisema.

Alisema Serikali itaendelea   kutoa taratibu za wageni ambao watashiriki, ambapo mpaka sasa wamepokea salamu  kutoka zaidi ya nchi 10, ikiwemo  Rais wa  China, XI Jingping. 

Alisema salamu zingine ni Uganda,Kenya,Afrika Kusini,Burundi na Zimbambwe.

Alisema burudani mbalimbali zitakuwepo katika sherehe hizo kama za ngoma za asili,wasanii muziki wa kizazi kipya.

“Niwaombe wananchi wa Dodoma na mikoa ya jirani tunaomba sana ifikapo saa moja kila mmoja awe amefika,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles