24.3 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Maambukizi ya Ukimwi yapungua nchini

RAMADHAN HASSAN-DODOMA

UTAFITI wa viashiria na matokeo ya Ukimwi wa mwaka 2016/17 unaonesha kwamba kiwango cha maambukizi ya VVU yamepungua kwa asilimia moja kutoka asilimia 5.1 mwaka  2011-2012 mpaka asilimia 5.0 kwa mwaka 2016/17.

Hayo yalimesemwa jana jijini hapa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Ajira, Kazi,Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama,  wakati akizindua utafiti huo.

Alisema utafiti huo unaonesha kwamba kiwango cha maambukizi ya VVU kwa watu wenye umri wa miaka 15-64 umepungua kwa asilimia moja kutoka asilimia 5.1 mwaka 2011-2012 na kufikia  asilimia 5.0 kwa mwaka 2016-2017 ambapo wanawake ni asilimia 6.5 na wanaume ni asilimia 3.5.

Waziri huyo alisema asilimia 60.9 ya watu wanaoishi na VVU ndio wanaofahamu hali zao ikiwa ni chini ya kiwango cha lengo ambapo amedai wamaofahamu hali zao asilimia 93.6 ndio wanaopatiwa dawa  za kufubaza makali ya VVU (ARV) ambao miongoni mwao asilimia 87.0 virusi vyao vimefubazwa.

Alisema utafiti huo unaonesha zaidi ya nusu milioni ya watu wanaoishi na VVU Tanzania hawajui hali yao ya maambukizi.

“Juhudi za pamoja za wenye wigo mpana zinahitajika kuwafikia watu wanaishi na VVU ambao bado hawajapima na kujua hali zao  nakuanza dawa,” alisema.

Waziri huyo alisema takribani watu 72,000 wanapata maambukizi mapya huku kiwango cha wanaume kujua maambukizi kikiwa kipo chini kuliko wanawake.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Harusi Said Suleimani, aliipongeza Serikali ya Muungano kwa kupambana na maambukizi mapya ya ugonjwa huo.

“Nitumie nafasi hii kuipongeza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada ambazo wanafanya kupambana na ugonjwa huu pamoja na maambukizi mapya,” alisema.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAID), Dk. Leonard Maboko alisema utafiti huo ni wa kitaifa na ulifanyika katika ngazi ya kaya kuanzia Oktoba  mwaka 2016 hadi Agosti 2017 ambapo lengo ni kufahamu hali ya mwitikio wa Ukimwi nchini.

Dk. Maboko alisema utafiti ulihoji kaya 14,811 zilizojumuisha watu zaidi ya 31,000 wenye umri wa miaka 15 na zaidi pamoja na watoto  zaidi ya 9000 wenye umri wa miaka 0 hadi 14.

“Matokeo ya utafiti yanajumuisha takwimu zinazoonesha idadi ya watu wanaioshi na VVU, wangapi wanapata maambukizi mapya kwa mwaka na matumizi ya afya kwa wanaoishi na VVU,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,476FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles