Safina Sarwatt, Siha
Maambukizi ya ugonjwa wa malaria umeripotiwa umeathiri kwa kiasi kikubwa katika Wilaya za Mwanga na Same na kuathiri watoto chini ya umri wa miaka mitano na wajawazito .
Mkuu wa Mkoa wa Dk .Anna Mghwira ameyasema hayo leo Juni 20 wakati akipokea mwenge wa uhuru katika kijiji cha Omelili wilayani Siha mkoani hapa ukitokea mkoani Manyara.
Amesema takwimu zinaonyesha hali maambukizi ya ugonjwa wa malaria ni asilimia moja na kwamba watoto chini ya miaka mitano na wajawazito wameathirika zaidi.
Amesema kutokana na hali hiyo mkoa umeendelea kutoa elimu na ushauri  kwa wananchi kwenye wilaya hizo kutumia vyandarua  na kufanya usafi katika maeneo yao ili kutokomeza masalia ya mbu.
“Mkoa umeendelea kupambana kupunguza vifo vitokanayo na malaria kwa kutoa elimu kwa wananchi kufyeka majani na kuondoa maji katika maeneo yanayowazunguka ili kuhakikisha masalia yote ya mbu yanatokomezwa,”amesema.
Mwenge wa uhuru utazindua jumla ya miradi 35 ikiwamo afya, elimu, barabara katika wilaya saba za mkoa wa Kilimanjaro yenye thamani ya Sh.bilion 41.3 .