25.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 17, 2021

Maambukizi mapya 8,855 yaripotiwa Urusi

MOSCOW, URUSI

URUSI imeripoti maambukizi mapya 8,855 ya virusi vya corona jana  na kufikisha idadi jumla ya walioambukizwa kuwa 458,689. 

Maofisa wa serikali wamesema watu 197 wamefariki ndani ya masaa 24 na kuleta pia idadi jumla ya vifo kufikia 5,725. 

Huku hayo yakiarifiwa maofisa wa afya nchini Malaysia wameripoti visa 38 vya maambukizi mapya, huku vifo vikiripotiwa kufikia 171. 

Watu 8,304 wameambukizwa virusi vya corona nchini Malaysia. 

Hadi sasa idadi ya walioambukizwa duniani imepindukia milioni sita huku vifo vikipindukia laki nne.

BOLSONARO ATISHIA KUIONDOA BRAZIL WHO 

Wakati huo huo, Rais wa Brazil Jair Bolsonaro ametishia kuiondoa nchi yake katika shirika la Afya Duniani (WHO), akichukua hatua sawa na iliyochukuliwa na Marekani kujitoa katika shirika hilo mwishoni mwa mwezi uliopita. 

Rais Bolsonaro amesema ama WHO ifanye kazi bila ubaguzi wowote wa kiitikadi au Brazil iondoke huku akisisitiza kuwa hawahitaji mtu yeyote kutoka nje kutoa ushauri kuhusu afya nchini humo. 

Rais Bolsonaro ameyasema hayo baada ya shirika hilo la afya ulimwenguni kuanzisha tena uchunguzi wa dawa ya hydroxychloroquine kwa wagonjwa wa COVID 19. Bolsonaro amesema haelewi ni kwanini shirika hilo lilionya kuhusu matumizi ya dawa hiyo kisha baadae kuamua kuanzisha tena uchunguzi wake kwa waathirika wa virusi vya corona. 

Marekani ilisitisha uhusiano wake na WHO baada ya Trump kudai imeshindwa kufanya mabadiliko ya haraka kuhusu namna inavyoshughulikia janga hilo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,567FollowersFollow
517,000SubscribersSubscribe

Latest Articles