23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Maalim Seif: mpango wa kuigeuza Singapore uko pale pale

Mwandishi Wetu, Zanzibar

Mwanachama namba moja wa Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema mpango wa kuigeuza Zanzibar kuwa Singapore bado anao.

Maalim Seif ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), amesema hayo leo Jumamosi Machi 23, alipokuwa akizungumza na wananchi wa eneo la Ngezi Chambani Wilaya ya Mkoani Kusini Pemba.

Mwaka 2015 katika kampeni za kuwania Urais Visiwani Zanzibar, Maalim Seif moja ya ahadi zake ni kugeuza visiwa hivyo kuwa kama Singapore kiuchumi.

Leo akizungumza na wananchi hao ambao awali walikuwa wanachama wa CUF na sasa wamejiunga na ACT amesema adhima yake hiyo bado ipo palepale.

“Baada ya mambo kwenda vibaya CUF sasa tumetafuta jahazi jingine ili aweze kufikia lengo hilo,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles