31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, December 12, 2024

Contact us: [email protected]

MAALIM SEIF KUMTEMBELEA LEMA GEREZANI

Na JANETH MUSHI-ARUSHA

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, leo anatarajiwa kumtembelea Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), anayeshikiliwa kwa zaidi ya miezi miwili katika mahabusu ya Gereza Kuu la Kisongo jijini Arusha.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili jana, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa, ambaye pia ni Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, alisema Maalim Seif alitarajiwa kutua jana katika uwanja mdogo wa ndege wa Kisongo na leo atamtembelea Lema.

“Leo (jana) tunaenda kumpokea uwanja mdogo wa ndege na kesho ataenda kumtembelea Lema, ila kwa kuwa ni kiongozi wa CUF, mambo mengi ya kiitifaki yatakuwa ya CUF, kwa hiyo akishafika kesho ndiyo tutajua anaenda muda gani pamoja na taratibu nyingine,” alisema Golugwa.

Desemba 31, mwaka jana mawaziri wakuu wa zamani ambao pia ni wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa na Fredrick Sumaye walimtembelea gerezani mbunge huyo.

Pia Desemba 11, mwaka jana, Katibu wa Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, alimtembelea Lema katika mahabusu hiyo na alimtia moyo aendelee na mapambano na kumtaka asikate tamaa ya kupigania haki za Watanzania.

Lema alikamatwa Novemba 2, mwaka jana akiwa nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma na kufikishwa mahakamani Novemba 11, mwaka jana akikabiliwa na kesi za uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli na hadi wakati huu bado anashikikiwa mahabusu ya gereza hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles