31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Maalim Seif: katika vyama vinne tulivyotaka kuhamia ACT imekidhi vigezo


Mwandishi Wetu

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharrif Hamad, amesema kabla ya kuhamia ACT-Wazalendo walifanya utafiti katika vyama vinne.

Amevitaja vyama hivyo kuwa ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), NCCR-Mageuzi, NLD na ACT yenyewe ambayo amedai ndiyo iliyokidhi vigezo walivyovihitaji na kisha kuhamia.

Akizungumza katika kipindi maalumu katika Televisheni ya mtandaoni ya Kwanza TV akiongozwa na Maria Sarungi, leo Jumatano Machi 20, Maalim Seif amesema walijenga urafiki kwa vyama hivyo huku wakiendelea na utafiti wao.

“Tulikuwa na vyama hivyo vinne, vitatu vilikuwa wenzetu katika Ukawa, ambao ni hao Chadema NCCR-Mageuzi na NLD,  ACT hawakuwa wanachama wa ukawa lakini walikuwa wameshaleta maombi ya kujiunga Ukawa.

“Tuliunda timu ya viongozi wetu na wote walikaribishwa kwa kila chama. Swali lilikuwa ni kwamba ikitokea sisi tunahama chama je mtatukaribisha?

“Wote walisema karibuni lakini tulikuwa na ‘criteria’ zetu je malengo yetu na yao yanafanana, baada ya kupima vigezo vyote hivyo, ni uamuzi uliokuwa mgumu kidogo lakini tukaona chama ambacho kimeanza kuaminika na wananchi hata kama ni kidogo tukachagua ACT-Wazalendo, katika vizuri basi kuna kizuri zaidi…” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,625FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles