27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

Maalim Seif awafariji wahanga wa uchaguzi

Na TALIB USSI – ZANZIBAR

MWENYEKITI wa chama cha ACT wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amefanya ziara maalum ya kuwatembelea ili kuwafariji wafuasi wa chama hicho ambao waliathriwa na kupigwa na watu wanadhaniwa kuwa ni vikosi vya ulinzi na usalama Zanzibar.

Maalim Seif amefanya ziara hiyo kwa mara ya kwanza tangu uchaguzi mkuu ulipomalizika Oktoba 28 mwaka huu.

Akiwa katika safari hiyo Mwenyekiti huyo aliungana na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar ambaye pia ni Katibu wa Habari na uenezi, Salim Biman katika maeneo tofauti mjini Zanzibar.

Katika ziara hiyo Maalim Seif aliwaomba waathirika hao kuwa wavumilivu na kutokana na majeraha hayo ambayo wameyapata na kudai kwa yamesababishwa na utawala ambao haujataka kufuata sheria.

Sambamba na hilo Malim Seif ambaye alikuwa mgombea wa Urais Zanzibar kupitia ACT Wazalendo alilitaka jeshi la Polisi kufuata misingi yao kazi wanapofanyakazi na sio kuwaonea raia ambao hawana hatia.

Maalim Seif alieleza kuwa matukio hyo yadaiwa kufanywa na vikosi vya ulinzi na usalama ni kinyume na haki za biaadamu kama wanaharakati wa haki za binadamu wanavyopiga kelele ulimwenguni kote.

 “Maalim tunajua kwa nini unateswa hivi ni kwa sababu tunataka haki na utawala bora, lakini nakuhaikishia hatutorudi nyuma hadi tulipate tunalolitafuta”  alisema Duni Ali Haji wa Makadara  Mjini Zanzibar.

Haji ambaye alipata kipigo kikali kilichosababisha mguu wake kuvunjika alisema alipata kipigo hicho wakati akiwa njiani kuelekea katika kituo chake cha kupiga kura.

“Yaani sijafika kiuoni kundi la askari na wengine waliofunika nyuso zao walinifuata na kunivamia kwa marungu” alisema Haji.

Chama cha ACT Wazalendo kimesema wafuasi wake zaidi ya 500 wamewekwa rumande kipindi hiki cha uchaguzi Visiwani Zanzibar wakiongozwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Nassor Ahmed Mazurui ambaye tangu tarehe 27 mwezi huu hajuilikani alipo licha ya Jeshi la Polisi Zanzibar kukiri wanamshikilia.

Pia baadhi ya wafuasi waliachiliwa bila kupelekwa mahakamani huku wengine wakiwa katika hali mbaya na kuhitaji matibabu nje  ya Zanzibar.

Watu wengi walioathirika na ukiukwaji wa haki za bnadamu Zanzibar pamoja na wale ambao hadi leo wanalazimika kukimbia nyumba zao na kukimbilia misituni wameitaka Jumuiya za kimataifa kuingilia katika na kuwachukulia hatua waliowatesa na kuwapiga watu kwa kisingizio cha kulinda amani wakati na baada ya uchaguzi.

Uchaguzi wa Zanzibar ulifayika tarehe 27 na 28 Oktoba mwaka huu na chama kikuu cha Upinzani Zanzibar kikipinga upigaji kura huo, hali ambayo ilisababisha jaribio la kuandamana na Polisi kujibu kwa nguvu kwa kutumia mabomu ya machozi na risasi za  moto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles