22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

Maalim Seif abanwa kila kona

Na MWANDISHI WETU

GWIJI wa siasa za upinzani visiwani Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ni kama amebanwa kila kona kisiasa, baada ya kuendelea kukutana na vigingi hata baada ya kuhamia chama kipya cha upinzani cha ACT- Wazalendo siku chache zilizopita.

Licha ya kulazimika kukiacha Chama cha Wananchi (CUF) alichokiasisi miaka 27 iliyopita kutokana na mvutano wa kisiasa ulioibuka kati yake na Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba, mara tu baada ya kumalizika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, safari yake ACT-Wazalendo nayo inaweza kuwa ya misukosuko.

Uthibitisho wa hilo ni dalili za mwanzo kabisa zilizoanza kujionyesha siku chache baada ya kuhamia chama hicho kipya akiwa na lundo la wafuasi wake. 

Hatua ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kueleza nia yake ya kukifutia usajili chama cha ACT-Wazalendo ikiwa ni takribani wiki moja tu tangu chama hicho kimpokee Maalim Seif na wafuasi wake, imejenga hisia kwamba mwanasiasa huyo bado anapitia njia ile ile.

Ingawa Ofisi ya Msajili haikueleza kama uamuzi wake huo unatokana na Maalim Seif kuhamia ACT-Wazalendo, lakini ilitaja mambo yanayodaiwa kukiukwa na chama hicho ikiwamo vitendo vya uvunjifu wa sheria kama kuchoma moto bendera za CUF baada ya Mahakama kutoa hukumu inayompa uhalali Profesa Lipumba kuwa Mwenyekiti halali wa CUF.

Zaidi barua hiyo ya Msajili kwenda ACT-Wazalendo iliyoandikwa Machi 26 mwaka huu, imekituhumu chama hicho kutumia dini katika …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles