23.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

Maagizo ya Mkuu wa Wilaya Serengeti yatekelezwa

Na Malima Lubasha, Serengeti

MAAGIZO aliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti,Kemirembe Lwota kwa uongozi wa Kijiji cha Nyami huru kilicho Kata ya Busawe ya kukutana na wananchi waliovamia eneo la kijiji la kujenga shule ya Sekondari na kuona jinsi ya kumaliza changamoto hiyo yametekelezwa kupitia vikao vya Kata,Tarafa na Kijiji.

Utekelezaji wa maagizo hayo yamethibitishwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Ayubu Makuruma wakati alipozungumza na Mtanzania Digital kuhusu hatua iliyofikiwa kutokana na kuchelewa kwa ujenzi wa Sekondari mpya yamefikiwa akisema yametekelezwa kupitia vikao vilivyohusisha wananchi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti,Ayubu Makuruma akizungumza katika baadhi ya vikao vya Halmashauri hiyo.

Amesema kuwa mkuu wa wilaya alifika katika kijiji hicho August 2, 2024 mwaka huu kuona maendeleo ya ujenzi wa shule mpya ya Sekondari ambapo alipokea taarifa ya baadhi ya wananchi kuwa wamejenga nyumba eneo hilo na wamegoma kuondoka hivyo alitoa siku saba kwa uongozi wa kijiji,kata na tarafa kukutana haraka kuona namna ya kumaliza changamoto hiyo ili ujenzi wa shule uanze.

Mwenyekiti huyo wa Halmashauri na Diwani wa Kata hiyo, amesema kufuatia maagizo hayo ya vikao vilifanyika kwa kushirikisha wananchi na wale waliovamia eneo hilo ambao wanafikia 19, kwa hiari walikubali kuondoka eneo hilo la kijiji ili ujenzi uweze kuanza na taarifa ya makubaliano kupelekwa kwa mkuu wa wilaya.

Makuruma amesema kuwa baada ya Serikali kutoa fedha kiasi cha Sh milioni 584,280.29 kwa ajili ya kujenga sekondari mpya taarifa zilifikishwa Serengeti.

“ Hilo lilikuwa ni eneo la shamba la kijiji tangu kuanzishwa kwa vijiji vya ujamaa likiwa na ukubwa wa ekari 130, wanakijiji walikuwa wakilima mazao kama vile pamba,mtama, ulezi,mihogo na mazao mengine pia kutenga maeneo ya miundombinu ya afya,elimu ofisi ya Kijiji lakini baadhi ya wananchi bila kujua au wakijua ni mali ya kijiji wakaamua kujenga makazi. Tunashukuru wamekubali kupisha kujengwa kwa sekondari na kuita jina la Kibaroti baada kutolewa elimu ya kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wao,”amesema Makuruma

Mwenyekiti huyo amefafanua kuwa kutokana na wananchi hao kupisha kwa hiari Mhandisi wa Halmashauri na wataalamu wanaohusika na sekta ya elimu wamefika eneo hilo na kuota maelekezo ya namna shughuli za ujenzi zitakavyofanyika hasa ujenzi wa madarasa, jengo la utawala,maabara,vyoo na miundo mbinu mingine ambapo ujenzi unatarajiwa kuanza muda wowote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles