28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Maafisa Utamaduni na Michezo kukutana Mei 22 kujadili maendeleo ya sekta hizo

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo inatarajia kuwakutanisha Maafisa Utamaduni na Michezo lengo ikiwa ni kujadili mikakati bora ya kuendeleza sekta hizo.

Akizungumza Mei 06,2021 katika mahojiano na Kituo cha Redio cha A FM Jijini Dodoma Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo nchini, Yusufu Singo ameeleza kuwa kikao hicho kitakua cha siku mbili na kitaongozwa na mada mbalimbali pamoja na kujadili utekelezaji wa Sera,Kanuni na Miongozo mbalimbali ya Sekta hizo.

 Hata hivyo, Mkurugenzi huyo alitumia nafasi hiyo kueleza kuwa  maandalizi ya Mechi ya Simba na Yanga itakayochezwa Mei 08,2021 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa yamekamilika.

“Habari na Michezo ni Sekta zinazotegemeana  sana  kwa  mfano mwisho wa juma hili  tuna mechi ya Simba na Yanga, bila  umma kuelezwa vizuri juu ya mechi hii inaweza kukosa msisimko” amesisitiza  Mkurugenzi Singo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles