23.6 C
Dar es Salaam
Friday, March 24, 2023

Contact us: [email protected]

Maadhimisho ya miaka 70 ya TNMC yazinduliwa Dodoma

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

MAADHIMISHO ya miaka 70 tangu kuzaliwa kwa Baraza la Uuguzi na Ukunga (TNMC)  yamezinduliwa Machi 17, 2023 jijini Dodoma ambapo wakazi wa Jiji hilo wamechangamkia  fursa ya kupima magonjwa bure katika viwanja vya Nyerere Square huku wataalamu wakishauri kujiunga na club za kuchangia damu nchini.

Katika madhimisho hayo Taasisi na Hospitali zinaendelea kutoa huduma mbalimbali zikiwemo CCBRT, Hospitali ya Rufaa ya Bugando, KCMC, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Muhimbili na Kibongoto.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika maadhimisho hayo, Afisa Uhamasishaji Damu salama Kanda ya Kat,i Bernadino Medaa  amesema wakazi wa Dodoma wamechangamkia fursa ya kujitokeza kwa wingi kuchangia damu.

Amesema wagonjwa wenye makundi ya damu ya RH-negative hupitia changamoto ya ukosefu wa damu wakati wa kuugua kwani baadhi yao hawawezi kuchangiwa damu na makundi mengine.

Licha ya uchache wa watu wenye makundi adimu ya damu, uwekezaji wa damu yao umetajwa kuwa muhimu.

“Japo watu sio wengi lakini wenye makundi O, A,B na AB negative wanapofika hospitali ugharimu maisha yao, kwahiyo tukiwapata tunawahamasisha kuingia kwenye uwekezaji wa damu. Kwa mfano wenye makundi ya O-negative yeye anaweza kumchangia damu mtu yeyote lakini yeye hawezi kuchangiwa,”amesema Medaa.

Akizungumzia maadhimisho hayo Kaimu Mkurugenzi wa Usajili, Leseni na Maadili, Jane Mazigo amesema wauguzi ni kada ya afya inayobeba asilimia 70 ya utendaji wa hospitali nchini.

Jane ametumia maadhimisho hayo kuwakumbusha wauguzi kufanya kazi kwa bidii na uwajibikaji ili kulinda leseni zao.

Mkazi wa Nkuhungu, Liberatus Manyasi amelipongeza Baraza hilo kwa kuandaa maadhimish hayo ambayo yameenda pamoja na upimaji wa magonjwa mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,070FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles