22.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, July 23, 2024

Contact us: [email protected]

M-BET kuwapeleka mashabiki wa soka Afcon Misri

Na Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya M-BET itapeleka mashabiki wa soka katika fainali ya Mataifa ya Afrika (Afcon) yaliyopangwa kuanza Juni 21 mpaka Julai 19 nchini Misri.

Hayo yalisemwa na Meneja Masoko wa M-BET Tanzania, Allen Mushi wakati wa kumzawadia Samwel Jonas mkazi wa Karatu, mkoa wa Manyara, aliyeshinda kitita cha Sh 125, 570, 420 baadaya kubashiri kwa usahihi michezo 12 ya droo ya Perfect 12.

Mushi alisema kuwa mashabiki wa soka wanatakiwa kubashiri mechi 10 na kuingia katika droo maalum ambapo washindi watakwenda Misri kuanzia mechi ya pili ya timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars dhidi ya Kenya ambayo itafanyika Juni 27.

Mushi alisema kuwa washindi hao pia watapa fursa ya kuona mechi ya mwisho ya hatua ya makundi ya Taifa Stars dhidi ya Algeria iliyopangwa kufanyika Julai Mosi.

Alisema kuwa kampuni yao itagharimia usafiri na gharama nyingine kwa mashabiki wake kuanzia nchini mpaka mjini Cairo pamoja na kutembelea vivutio vya utalii.

Mbali ya mashabiki wa soka kwenda Misri, M-Bet pia itawazawadia watanzania zawadi ya jezi kwa mashabiki wa soka watakaoweza kucheza tiketi tatu katika michezo yoyote.

Wakat huo huo: Mushi alisema kuwa M-Bet imeendelea kuwa nyumba ya mabingwa baada ya kumzawadia mshindi wa sita kitita sh Sh milioni 125.7, shabiki wa Chelsea na Barcelona, Samwel Jonas (26).

Mushi alisema kuwa M-Bet imeendelea kuwa nyumba ya mabingwa wa kuwezesha Watanzania kupitia michezo yao na kuwajaza mamilioni ya fedha.

“Jonas ni mshindi wa sita mwaka huu. Hii inadhihirisha kuwa sisi ni nyumba ya mabingwa kwani washindi wanazidi kupatikana. Tunawaomba mashabiki kuendelea kucheza michezo yetu ili kuinua kipato chao,” alisema Mushi.

Kwa upande wake, Jonas alisema kuwa amefarijika sana kushinda fedha hizo na atafanyia uwekezaji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles