25.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Lwakatare ang’atuka ubunge

RAMADHAN HASSAN -DODOMA

MBUNGE wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare (Chadema), ametangaza hatagombea tena ubunge katika Jimbo la Bukoba Mjini huku akidai kwamba anaondoka akiwa hana deni lolote.

Lwakatare anaungana na Mbunge wa Kuteuliwa, Alhaj Abdallah Bulembo na Mbunge wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM) ambao wametangaza kutogombea tena ubunge.

Mbunge huyo anakuwa ameongoza jimbo hilo kwa miaka kumi.

Akichangia jana mjadala wa bajeti ya Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa mwaka 2020-2021, Lwakatare alilishukuru Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Bukoba Mjini kwa kufanya nao kazi vizuri.

“Shukrani zangu nimshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ananisimamisha hapa nachangia kwenye wizara hii, mimi kwa miaka 13 nimekuwa mtumishi, nimekuwa ofisa utumishi na utawala.

“Leo hii nashukuru Mungu nafuata nyayo za mama  Tibaijuka (Anna) na Mheshimiwa Bulembo (Abdallah) wanaotaka mkondo wa Kagera kuomba kupumzika katika siasa ambazo nimezitumikia kwa miaka mingi, mimi kwahiyo namshukuru Mungu.

“Kwa hiyo niseme mimi sina deni, waliowahi kunishinda wamenishinda, namaliza Bunge nikiwa nimewashinda na ninaamini nimejenga upinzani ‘credible’ ambao unaweza kuendelea kuiongoza Halmashauri ya Bukoba.

”Na tumeonyesha kwamba upinzani wanaweza kufanya kazi bila migogoro na kwa kusikilizana na niwashukuru kabisa madiwani wa Bukoba wa vyama vyote kwani tumeendesha halmashauri tukiwa tunashirikiana.

”Pamoja na viongozi wote wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa ninawashukuru sana sana,” alisema Lwakatare. Akichombeza Naibu Spika, Dk.Tulia Ackson alisema: ”Mheshimiwa na sisi tukutakie kila la heri katika maisha yako mpya utakayoanza, tukiamini kwamba hutachukua fomu maana kuna watu wanaaga lakini wanarudi tena, tunakutakia kila heri.”

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,526FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles