25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Lusinde amtaja aliyeweka kiwango cha tozo miamala ya simu

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

MJUMBE wa Halmashauri Kuu Taifa CCM (MNEC) na Mbunge wa Jimbo la Mvumi mkoani Dodoma, Livingstone Lusinde, amefunguka kuhusu makato ya miamala ya simu kuwa Bunge lilipitisha sheria lakini kiwango kilipagwa  na  Waziri wa Fedha na Mipango, Mwigulu Nchemba, hivyo wabunge wasilaumiwe.

Amesema mjadala kwa sasa uwe tozo ni kubwa, hivyo Waziri apunguze na lisilaumiwe Bunge kwa kupitisha sheria hiyo kwani hata mwanzo makato yalikuwepo na watu  walikuwa wanalipa.

Lusinde amedai Wabunge wanakatwa kodi ambazo zinaenda kwenye shughuli za kimaendeleo hapa nchini hivyo jamii ipuuze  maneno kwamba wao hawakatwi.

Akizungumza leo Agosti 3,2021 na waandishi wa habari mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu, amesema Bunge wametunga sheria na wala sio kiwango kwani hilo ni jukumu la Waziri wa Fedha na Mipango.

“Sisi tumetunga sheria sio kiwango, mbona hata mwanzo makato  yalikuwa kwenye simu, kiwango anapanga Waziri na wanatengeneza kanuni nina uhakika makato  yatapungua ndugu zangu tujifundishe kulipa kodi nani wa kutupa hela za  bure?Mjadala uwe hapo tozo ni kubwa hivyo Waziri apunguze sio lilaumiwe Bunge,”amesema.

Kuhusiana na mishahara yao kukatwa kodi,Lusinde amesema wao wanakatwa kodi ambazo zinaenda kwenye shughuli za kimaendeleo hapa nchini hivyo jamii iondokane na maneno kwamba wao hawakatwi kodi.

Mbunge huyo amedai kwamba Wabunge wanalipwa shilingi milioni 4.6 kwa mwezi huku makato ya yakiwa ni zaidi ya milioni 1.2 hivyo anashangaa kusikia kwamba Wabunge hawakatwi kodi.

“Nilitaka nizungumze hoja ambayo imeibuliwa na Mzee Utoah(Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,Mstaafu) sijaelewa Mzee Utoah anataka kuzungumza nini mtu ambaye amewahi kuwa CAG hajui kwamba tunalipa kodi

“Ndugu zangu mimi nimeleta hapa ‘salary sleep’ yangu mimi Livinstone Lusinde  umeelezwa hapo kodi yangu imeelezwa hapo sasa mtu anaposema hili ni jambo la aibu sana.

“Mtu anayesema wabunge hatulipi kodi ni mtu wa wapi? Nchi ya wapi haya ni maneno ya uzushi  kwa kuwa namheshimu sisemi nilitaka kusema amesema uongo ila sisemi,”amesema.

Mbunge huyo amesema wale wanaoona kazi ya ubunge ni rahisi wajaribu kugombea kwani mwaka 2025 sio mbali.

Amesema hata kwenye miamala ya simu Wabunge ndio wamekuwa wakilipa fedha nyingi kutokana na wananchi wengi kuwa na shida hivyo kutuma kwa kutumia simu.

Kuibuka kwa  Lusinde, ni baada ya hivi karibuni Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa, akiwa katika  mkutano wa hadhara uliowashirikisha Wananchi wa Mzinga Ukonga Jijini Dar es Salaam  kudai Wabunge waanze kulipa kodi kupitia mishahara yao ili wapate uwezo wa kuwaambia Wananchi na wao walipe kodi.

Pia hivi karibuni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mstaafu, Ludovick Utouh, alisema wabunge hao wanatakiwa kukatwa kodi katika mishahara yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles