21.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Lupita Nyong’o sasa hii sifa!

New York, Marekani

NYOTA wa filamu nchini Marekani mwenye asili ya Kenya, Lupita Nyong’o, ameonesha jeuri ya fedha kwa kuvaa mavazi yenye thamani ya dola milioni 3.5, zaidi ya bilioni 8 za Kitanzania kwenye tuzo za SAG 2020.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 36, ambaye aliwahi kutwaa tuzo za Oscar, alikuwa mmoja kati ya mastaa ambao walivaa mavazi yenye thamani kubwa ikiwa pamoja na Jennifer Lopez.

Lupita alikuwa amevaa gauni la Louis Vuitton lenye rangi nyeupe kidogo na nyeusi likiwa na vipande 32,000 vya madini ya almasi kwa ajili ya kung’arisha nguo hiyo. Kwa upande wa Jennifer Lopez, yeye alionesha jeuri ya fedha kwa kuvaa mavazi yenye thamani ya dola milioni 9, ambazo ni zaidi ya bilioni 20 za Kitanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,656FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles