MKALI wa filamu nchini Kenya, Lupita Nyongo, amepania kufanya makubwa kwa mwaka 2016 ili kuweza kutangaza jina lake zaidi.
Mrembo huyo ambaye aliwahi kuchukua Tuzo ya BET mwaka 2014 na Tuzo za Oscar mwaka 2015, amekuwa akifanya vizuri katika filamu na sasa amekuja kivingine katika filamu mpya ya ‘Star War’.
“Ninahitaji kufanya makubwa kwa mwaka 2016 hasa katika maisha ya filamu, najua kwamba kuna ushindani wa hali ya juu lakini natakiwa kupambana ili kuzidi kutangaza jina langu zaidi ya miaka iliyopita.
“Yote yanawezekana kikubwa ni kujipanga vya kutosha ili kuhakikisha natimiza malengo yangu, watu wanasema ninafanya vizuri lakini kwa upande wangu ninasema kuwa bado nina safari ndefu,” alisema Lupita