26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Lupinga:Wakuu wa mikoa jiepusheni na rushwa

HARRIETH MANDARI-GEITA

KATIBU wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kanali mstaafu, Ngemela Lubinga amewataka wakuu wa mikoa kuchapa kazi na kuachana na vitendo vya rushwa.

Alitoa kauli hiyo juzi kwenye kikao cha wakuu wa mikoa 10 wa kanda ya ziwa na magharibi  ambao walikutana mkoani Geita katika kikao cha ujirani mwema   kujadili hali ya usalama katika mikoa hiyo na kuweka mikakati  utendaji.

Mikoa hiyo ni Tabora, Kigoma, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Singida, Kagera, Rukwa, Katavi, Mara na Geita.

Vilevile  walipata fursa ya kutembelea miradi  mbalimbali iliyojengwa kupitia fedha za  miradi ya  jamii ( CSR),  ikiwamo  zahanati  ya Nyamalembo,  Shule ya Msingi Bombambili, kiwanda cha kuchakata dhahabu  cha Magambo  na mgodi wa GGML.

Alisema umefika wakati wa kuchapa kazi na kuhakikisha wanawajibika kwa ufanisi   katika majukumu yao   ikiwamo kutunza siri za Serikali.

“Tuwajibike kwa ukamilifu kwa kuhakikisha mnasimamia  migogoro iliyopo maeneo yetu.

“Epukeni  rushwa kuna watu wanatumia nafasi zao vibaya wanashidwa kusimamia ipasavyo wanapokea rushwa.

“Mkuu wetu wa nchi anapenda watu watendewe haki na imani yake ataka tuishi mazingira ya amani,”alisema.

Aliwashukuru kuanzisha ushirikiano wa ujirani mwema, kwa sababu  unaleta  chachu ya maendeleo katika mikoa yao.

Aliwataka kuendelea kusimamia ilani ya  CCM, na pia kuwatumikia wananchi kwa ukamilifu.

Mwenyekiti wa kikao  hicho ambaye ni Mkuu wa Mkoa  wa Tabora, Aggrey Mwanri, alisema lengo la kikao hicho lilikuwa kujifunza na kubadilishana  uzoefu wa mbinu mbalimbali za  utendaji katika nyanja za  uchumi na utawala bora.

Alisema haiwezekani nchi tajiri kama  Tanzania wageni  waingie na  kusomba mazao kama vile  alizeti  ambyo huisafirisha  kwenda kuiboresha nchini mwao kwa manufaa yao, badala ya kuongeza thamani hapa   nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles