24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

Lulu sasa huru kufanya yake, amaliza kifungo chake

Na Anna Potinus , Dar es salaamMsanii Elizabeth Michael (Lulu) leo Novemba 12 anamaliza kifungo chake tangu alipohukumiwa miaka miwili gerezani kuanzia Novemba 13 na baadaye kubadilishiwa kifungo cha nje alichokuwa akikitumikia kwa kufanya shughuli za kijamii.

Baada ya kumaliza kifungo hicho msanii huyo atakuwa huru kuendelea na shughuli zake tofauti huku wengi wakimtabiria kurudi katika shughuli yake ya sanaa ya uigizaji wa filamu.

Msanii mwenzake, Mahsein Awadhi maarufu Dokta Cheni, ameonyesha furaha yake kwa kuandika ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram akimtaka msanii huyo amshuru Mungu kumaliza kifungo hicho salama na anamtaka aendelee  kumuomba Mungu.

“Sina la kusema @elizabethmichaelofficial zaidi ya kumshukuru Mungu na kumwambia Mungu asantee kwa hili jambo kuisha salama, unajua jinsi gani lilituumiza kichwa ila Watanzania wenye mapenzi mema na wewe walikuombea kila saa,

“Sasa wakati mwengine unaenda kuanza maisha upya na mapya karibu uraiani tuje kupambana wote na imani Mungu anaenda kukutendea miujiza mikubwa katika maisha yako,” ameandika Dokta Cheni na kuendelea.

“Mwanzo tuliona ni muda kama hauwendi kumbe kila kitu ukimwachia Mungu siku zinakimbia kuliko, kweli Mungu ni mwema natumai @elizabethmichaelofficial umemuona Mungu ajakuacha nikuombe nawe usimwache Mungu,”

Dokta Cheni ameendelea kuwashukuru wote waliokuwa nao kwenye kipindi muhimu na kigumu huku akiwaomba waendelee kumuombea zaidi huku akimshukuru pia mpenzi wa msanii huyo maarufu kwa jina la Dj Majizo.

“Nikushukuru sana tena sana baba mkwe mtarajiwa @majizzo we mtu una roho ya kipekee sana mtu akikutazama kwa nje anaweza asipate jibu ila moyo wako niwakipekee sana nimejifunza kitu kutoka kwako ila la mwisho kwako @majizzo nikukumbushe ile pete isiwe mwisho wa safari yenu naomba taratibu za mwisho ziendelee haraka japo najuwa kwako hilo halina tatizo ili ndoa ipite sasa dogo yupo Huru,” ameandika Dokta Cheni.

Lulu Michael alikuwa akikabiliwa na kesi ya kumuua Steven Kanumba bila kukusudia, kinyume cha kifungu cha 195 cha kanuni za adhabu, Aprili 7, 2012, Sinza Vatican jijini Dar es Salaam kufuatia ugomvi wa kimapenzi ulioibuka baina yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,208FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles