22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

LULU DIVA: SIKUBAHATISHA KUFANYA MUZIKI

NA ESTHER GEORGE


MSANII chipukizi anayefanya vizuri kwenye muziki nchini, Lulu Abasi ‘Lulu Diva’, amesema hakubahatisha kujitosa katika fani hiyo ila ana kipaji.

Lulu Diva ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa Usimuache, alisema hafanyi muziki kwa kuuza sura au kujionyesha kwa watu kuwa ilimradi anaimba, bali anajua anachokifanya na ana mipango ya kupiga hatua zaidi kimuziki.

“Sijabahatisha kufanya muziki kwani kipaji ninacho na naamini siri kubwa ya kufanya vizuri ni kuwa na malengo na kujituma, hivyo napambana kutengeneza nyimbo nzuri za kuelimisha.

“Lengo langu kubwa ni kufanya muziki wa kimataifa, naamini ninaweza kufanya hivyo kwa kuwa nina kipaji hicho, mashabiki wakae tayari kuendelea kupata kazi zangu mpya,” alisema Lulu Diva.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,220FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles